Mgombea Urais kupitia ACT Wazalendo Bernard Membe akikabidhiwa fomu na Mwenyekiti wa NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage, na wa kwanza kushoto ni Mgombea mwenza Profesa Omar Hamad.
Mshauri Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo, Bernard Membe, amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), zilizopo jijini Dodoma.
Membe amewasili kwenye ofisi za NEC hii leo Agosti 7, 2020, akiongozana na Katibu Mkuu wa chama hicho Ado Shaibu, Mgombea Urais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na mgombea mwenza Profesa Omar Hamad.
Wagombea wengine wa nafasi za Urais waliochukua fomu hii leo ni pamoja na Muttamwega Mgaywa, kutoka chama cha Sauti ya Umma (SAU), Queen Sendiga kutoka chama cha ADC pamoja na Twalib Kadege kutoka chama cha UPDP.
Zoezi la uchukuaji wa fomu hizo kwa wagombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu ujao, litahitimishwa Agosti 25 mwaka huu.
CHANZO - EATV
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464
CHANZO - EATV