Mgombea
ubunge kupitia chama Cha Mapinduzi CCM Boniface Butondo akisalimiana na
wananchi wakati akirejesha fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Kishapu
mkoani Shinyanga
Na Suzy Luhende -Shinyanga
Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kimeahidi kuendesha kampeni za kistaarabu katika kipindi chote cha kampeni, huku kikiwataka wanachama wake kutofanya vitendo vyovyote vyenye viashiria vya kuleta vurugu kipindi cha kampeni za kuwanadi wagombea udiwani na ubunge.
Ahadi hiyo imetolewa leo na Kaimu Katibu wa CCM Wilaya ya Kishapu, Jamal Khamis wakati mgombea ubunge kwa Jimbo la Kishapu kwa tiketi ya CCM, Boniface Butondo akirejesha fomu zake kwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Emmanuel Matinyi.
Khamis amesema CCM kitanadi kwa wananchi Sera na Ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2020 – 2025 katika hali ya amani na utulivu ambapo kimetoa wito kwa wanachama wake kujiepusha na kutoa kwa watu wengine kauli zisizokuwa za kistaarabu zinazoweza kuwa chanzo cha kutokea kwa vurugu.
Ahadi hiyo ya CCM ilionekana dhahiri baada ya wafuasi wa chama hicho na wale wa CHADEMA kuwasili wakati mmoja kwa mpsimamizi wa uchaguzi wakati wagombea wao wakirejesha fomu zao za kuomba uteuzi wa kugombea ubunge katika jimbo la Kishapu ambapo hakuna vurugu zozote zilizotokea.
“Tutafanya kampeni za kistaarabu zisizo kuwa na bughudha ambazo hazitashambulia mtu kampeni zenye malengo na kushawishi wapiga kura wetu waweze kutuchagua, tunaamini maendeleo msingi wake ni amani, pasipokuwa na amani hakuna maendeleo, naamini sisi tumejipanga kuwa na Kishapu mpya, yenye maendeleo mapya,” ameeleza Khamis.
Kwa upande wake mgombea ubunge jimbo la Kishapu kwa tiketi ya CCM, Boniface Butondo amekishukuru chama chake kwa kumteua kupeperusha bendera ya CCM na kwamba anaamini ataitetea vyema bendera hiyo kwa kukiletea ushindi chama chake.
Naye Msimamizi wa uchaguzi katika Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Emmanuel Matinyi amewataka wafuasi wote wa vyama vya siasa vitakavyosimamisha wagombea katika uchaguzi wa mwaka huu kuhakikisha vinafanya kampeni za kistaarabu zisizokuwa na aina yoyote ya vurugu ama kushambulia watu wengine.
“Tunaomba mtakapoanza kampeni kesho (Jumanne) naomba mfanye kampeni za kistaaribu, na hasa ninyi kama chama chenye Serikali mna wajibu mkubwa wa kuonesha utii wa sheria, hasa upande wa kuzingatia ratiba zenu za kampeni, hapo ndipo penye tatizo kubwa, hivyo ikitokea mabadiliko tuarifiane mapema,” ameeleza Matinyi.
Katika hatua nyingine wafuasi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo wamekutana pamoja katika ofisi za Msimamizi wa uchaguzi wakati wagombea wao wa ubunge walipokuwa wakirejesha fomu za kuomba uteuzi wa kugombea Jimbo la Kishapu.
Hata hivyo wafuasi wa vyama vyote viwili walionesha hali ya furaha na hapakutokea aina yoyote ya kurushiana maneno mbali ya upande wa CCM kudai wenzao baada ya kuwaona walisalimu amri kwa kukaa kimya wakiangalia shamra shamra zilizokuwa zikifanywa na wafuasi wa CCM ambao hata hivyo waliamua kukaa pembeni ili kutoa nafasi ya wenzao wa CHADEMA kuweza kuondoka katika eneo hilo.
Msimamizi wa uchaguzi katika Jimbo la Kishapu, mkoani Shinyanga, Emmanuel Matinyi amewatangaza wagombea wa CCM, Boniface Butondo na Idd Salum wa CHADEMA kuwa wagombea wa Jimbo hilo ambapo mgombea wa NCCR – Mageuzi, Zacharia Lugwila ambaye hata hivyo mpaka jana mchana alikuwa hajarejesha fomu zake.
Wafuasi wa CCM wilaya ya Kishapu wakimsindikiza mgombea wa ubunge kupitia CCM Boniface Butondo akirudisha fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga

Mgombea ubunge kupitia CCM Akimkabidhi msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Kishapu Emmanuel Matinyi fomu ya kugombea ubunge Jimbo hilo leo.