Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akitoa maelekezo kwa uongozi wa Mgodi wa ZEM uliopo eneo la Mahiga kata ya Mwakitolyo wilayani Shinyanga.
Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Shinyanga ikiwa chini ya duara lililojengwa kisasa zaidi wakikagua maendeleo ya mradi huo eneo la Mahiga Kata ya Mwakitolyo.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mh Jasinta Mboneko ametembelea na kukagua Mradi wa Uchimbaji wa Madini aina ya Dhahabu eneo la Mahiga Kata ya Mwakitolyo ambapo amtembela maduara ya kisasa yatakayotumika kwa shughuli
mbalimbali ikiwemo kuingiza magari kwa ajili kutolea mawe pamoja na kuingiza hewa safi kwenye mashimo hayo.
Mradi huo unaotekelezwa na kampuni ya ZEM Development ya Nchini Uchina Katika eneo la Mwakitolyo halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Ramadhan Bunyese ambaye ni Mlipuaji wa Miamba katika eneo hilo amesema kuwa kwa sasa wako katika uchorongaji wa Miamba ili kufanya uchimbaji kuwa rahisi.
“Uchimbaji huu tunaufanya kutoka juu hadi chini tunatarajia
kwenda umbali wa mita mia moja na
hamsini kutoka juu hadi chini ya ardhi
kisha tutaziunganisha ili kuwezesha mawasiliano kwa pamoja hivyo tunajitahidi
kwenda kwa kasi ili mwezi wa Sita Mwakani tuanze uzalishaji” amesema Ramadhan
Muhandisi wa Madini toka ofisi ya madini Mkoani Shinyanga
Gilliard Luyoka amesema kuwa uchimbaji huo umefuata hatua zote za serikali, ikiwemo utoaji wa vibari kwa kila hatua wanayofikia ikiwemo ukaguzi wa idara
ya mazingira toka ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira NEMC sambamba na ujengwaji wa Bwawa litakalotumika kumwaga taka zitakazotoka kwenye processing
Plant.
Kwa upande wake Meneja Miradi wa ZEM DEVELOPMENT Kevin Wang
amebainisha kuwa kutokana na makubaliano yao
kabla ya kuanza utekelezaji wa mradi huo ilikuwa ni kushiriki kuchangia
shughuli za maendeleo ndani ya kijiji na Kata ya Mwakitolyo hususani katika
Sekta ya elimu, afya n.k ambapo tayari wamekwisha changia ujenzi wa jengo la
serikali ya kijiji.
“Ni Jukumu letu kuwajibika kwa Jamii kwa kuchangia shughuli
za maendeleo ambapo tayari mwaka jana tumechangia ujenzi wa ofisi ya kijiji na mwakani tunajenga Jengo la
huduma za Nje OPD katika Zahanati ya mwakitolyo”
Wang ameongeza kuwa
katika makubaliano yao ni pamoja na
kujenga shule ya Msingi,huduma za kijamii ambapo wamehaidi kushiriki moja kwa moja
ambapo wamehaidi pia kuchangia miradi
mbalimbali ya maendeleo .
"Tuko mbioni kuonana na uongozi wa Wilaya chini cha Mkuu wa Wilaya pamoja na Mkurugenzi ili kuelezea mambo muhimu ya maendeleo"
"Tuko mbioni kuonana na uongozi wa Wilaya chini cha Mkuu wa Wilaya pamoja na Mkurugenzi ili kuelezea mambo muhimu ya maendeleo"
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Bi Jasinta Mboneko ameutaka
uongozi wa mgodi huo kuanza uchangiaji wa shughuli za maendeleo eneo hilo la
Mwakitolyo na kwa serikali kwa ujumla ambapo awali walibainisha baada ya eneo hilo kupatikana wataanza kulipa kodi ya
halmashauri ambayo wamewatakiwa kuanza kulipa.
“Hii ni sehemu ya makubaliano katika Mkataba wenu hivyo
lazima muanze kulipa halmashauri ili iweze kupata fedha toka kwenu hapa, lakini
pia kwa sababu mnaishi na jamii kuna vitu viko kwenye makubaliano ikiwemo
ujenzi wa Shule,Hospital na hata ulinzi hivyo lazima mshiriki kwenye shughuli
hizi siyo kungoja muanze uzalishaji mwakani”
Mboneko ameongeza kuwa kutokana na idadi kubwa ya wakazi wa
Mwakitolyo kutokana na shughuli zinazoendelea
lazima kuwepo kwa kituo cha polisi ambacho kitasaidia kuimarisha ulinzi na usalama na kuwataka wadau wote wa
maendeleo wakiwemo wachimbaji, blockers na mgodi huo wa ZEM kuchangia ili
kurahisha upatikanaji wa fedha zitakaoendeleza jengo ambalo limeishia kwenye msingi.
“Nakuagiza afisa mtendaji wa kata hii ya Mwakitolyo (WEO) kuhakikisha kuwa
ifikapo mwishoni mwa mwezi huu August 30 wadau wote wawe wamechangia ili tuweze
kujenga kituo cha polisi ili
kuimarisha ulinzi wenu hapa”
Mboneko ametembelea na kukagua maeneo pamoja na Blockers
waliopo mwakitolyo huku akizungumza na wachimbaji wadogo, blockers pamoja viongozi wa mgodi wa ZEM uliopo eneo la Mahiga.
Meneja Miradi wa ZEM Development Bw Kevin Wang akiongea na kamati ya usalama na ulinzi ikiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo Jasinta Mboneoko
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta mboneko akiteta jambo juu ya uhifadhi wa Mazingira
Mojawapo ya Maduara ya Kisasa ya uchimbaji wa Madini ya Dhahadu katika Mgodi wa ZEM uliopo Mahiga Mwakitolyo
Gilliard Luyoka muhandisi wa madini toka ofisi ya madini akitoa maelezo ya namna wanavyosimamia sheria za madini
Mkuu wa wilaya ,kamati ya ulinzi na usalama pamoja na uongozi wa mgodi wa Zem wakikagua maeneo mbalimbali ya mgodi huo.
Mlango wa kuingia kwenye moja ya maduara ya Zem Mahiga Mwakitolyo
Baadhi ya wafanya kazi wa Mgodi wa ZEM wakiendelea na kazi
Tazama picha mbalimbali za Matukio ya ziara ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Shinyanga ikongozwa na mkuu wa wilaya hiyo Jasinta Mboneko katika eneo la Mwakitolyo
Mkuu wa Polisi wilaya yShinyanga (OCD) Kafumu Lutonjaa