Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Shinyanga , Debora Magiligimba alipokuwa akiongea na wananchi wa wilaya ya Kahama katika mkutano wa hadhala wa kusikiliza kero zao uliofanyika kwenye uwanja wa shirika la nyumba mjini Kahama.
Na Patrick Mabula Kahama
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Shinyanga ,Debora Magiligimba amesema dhamana hi haki ya kila mtu na kuwataka wananchi wasiwe wanatoa rushwa kwa askari polisi wanapodhamini ndugu zao kwa sababu n kisheri.
Akiongea na wananchi kwenye mkutano wa hadhala juzi mjini Kahama alisema pia katika swala la kutoa dhamana nae askari polisi nao hawatakiwi kuomba rushwa kwa mtu yeyote anayetaka dhamana kwa mjibu wa sheria.
Magiligimba alisema askali polisi yeyote hatakiwi kuomba rushwa kwa mwananchi yeyote anateka dhamana kwa ndugu na jamaa yake kwa sababu kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na ni kosa ndani ya jeshi la polisi.
Alisema mwananchi yeyote atakayenyimwa dhamana au kutoridhika na huduma aliyopewa na askari aliwataka kuwaona viongozi polisi wa ngazi ya juu na kutoa taarifa yao kwa atakayotendewa pamoja na swala la kuombwa rushwa.
Magilingimba alisema kwa upande wao nao wananchi wasiwe chanzo cha kuwashawishi askali polisi kupokea rushwa katika kuwahudumia kwa sababu kufanya hivyo ni kosa la kisheria na kuwataka kutojihusisha na vitendo hivyo.
Kamanda Magiligimba alisema jeshi la polisi limejipanga kutoa huduma bora kwa wananchi na kuwataka wajikite katika kutoa taarifa za kuzuia uharifu mapema badala ya kusubiri ufanyike ndiyo watoe ripoti kituo cha polisi.
Aidha katika mkutano huo alitoa onyo kari kwa jamii kuacha mara moja kitendo cha kuwa wanajichukulia sheria mkononi cha kuwa wanaua watu wanapowakamata kwa tuhuma mbalimbali kwa sababu kufanya hivyo ni kosa kisheria na kuwataka wawe wanawapeleka kituo cha polisi au kwenye ofisi za serikali za mitaa , vijiji , kitongoji.
Kwa upande wao wananchi waliofika kutoa malalamiko na kero yao walisema bado kunavitendo vya rushwa kwa baadhi ya askali polisi ,hasa pale wanapotaka kuwadhamini ndugu na jamaa zao pamoja na swala la kuwababika kesi kwa watu.
Mmoja wa wananchi hao Donarld Masele alisema kilio chake ni askali polisi walipomkamata kwa kosa la kubambikwa na mtendaji wa kata ya Majengo mjini Kahama kisha kumfikisha kituoni walimnyimwa dhama licha ya kwaona viongozi wa juu wa polisi .
Akijibu hoja hizo kamanda Magiligimba alisema malalamiko na kero zote za wananchi walizotoa katika mkutano huo atazifanyia kazi , kwa sababu jeshi la polisi limejipanga kutoa huduma bora kwa jamii na kuwaomba waendelee kutoa ushirikiano katika kupambana na vitendo vya uharifu na rushwa ndani ya jeshi.
Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga ACP Debora Magiligimba akiwaasa wananchi wa mji wa Kahama kuacha kujihusisha na matendo maovu.
Mwananchi wa mtaa wa Majengo mjini Kahama Donarld Masele aliyesimama kulia alipokuwa akitoa kelo na malalamiko yake mbele ya kamanda wa polisi wa mkoa wa Shinyanga Debora Magiligimba
Kamanda wa Polisi,Mkoani Shinyanga ACP Debora Magiligimba akiwa na kamati yake ya usalama
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464