Mwenyekiti wa Baraza la Wanaume wa Kanisa la IEAGT Shinyanga, Haruni Mghuna akitoa neno kwa waumini wa kanisa hilo
Na Shinyanga Press Club Blog
KATIKA kuwasaidia wafanyabaishara na wajasiriamali mbalimbali mjini Shinyanga, Kanisa la International Evangelical Assembly of God Tanzania(IEAGT) limeitumia ibada ya Jumapili Agosti 23, 2020 kuwafundisha waumini jinsi ya kutumia nguvu ya ulimi katika kufanya biashara zao.
Mahubiri hayo yalifanyika katika kanisa hilo lililopo Jomu Manispaa ya Shinyanga, yakiongozwa na Askofu David Mabushi ambapo wafanyabiashara wa kanisa hilo walifundishwa namna ya kutumia ulimi wao vizuri ili kuweza kupata mafaniko zaidi katika biashara zao na kuacha dhana ya kukata tamaa na kulalamika kila siku.
Askofu Mabushi aliwaeleza wafanyabiashara kuwa hali ya kutotumia ulimi wao vizuri katika biashara kunaleta matokeo mabaya ya kutofanikiwa kwa kuwa wanashidwa kushawishi wateja wao juu ya bidhaa wanazouza.
Askofu David Mabushi
Mabushi aliwaasa wafanya biashara kujiamini na kupenda kazi zao wanazofanya licha ya hali ya mitaji yao kutofautiana ukubwa na mazingira wanayofanyia kazi.
Aliwashauri pia kutoacha kutoa maneno au kauli zenye picha ya kushidwa mara kwa mara katika hatua zote za biashara kwani kauli za kukiri kushidwa matokeo yake ni kushidwa moja kwa moja na kuanza kusema wachawi wameniloga.
"Mchawi wa kwanza wa mtu ni kauli zake mwenywe za kukiri mazingira ya kushidwa kila wakati na kujiona hafai kwa kila kitu," alieleza.
Mabushi alisema akinamama wengi wanaanguka katika biashara zao kwa kuwa wanakuwa wepesi kukiri kauli za kukatishwa tamaa na marafiki na ndugu zao wa karibu na kuacha kabisa kufanya biashara na hatimaye kujikuta wanaishi maisha ya tabu.
Pia aliwaomba akina mama kuwa katika mazingira ya utanashati na usafi ili kuweza kuwavutia wateja wao.
"Nawaombeni wa wanawake mjitahidi kuvaa vizuri ili wateja waweze pia kuamini na kupenda bidhaa zenu," alisema.
Mabushi alisititiza kuwa wafanyabiashara kuwa na maelezo ya kutosha juu ya faida ya bidhaa/huduma wanazouza uza ili kusaidia mteja kuamini kile anachokifanya kuwa ni sahihi.
"Kumekuwa na tatizo kubwa Sana,wengi wafanyabiashara hawana maelezo ya kina ya faida ya bidhaa/huduma na kujikuta wanakosa kuaminika kwa wateja wao"
Askofu Mabushi alibainisha kuwa hali ya kuwepo migogoro baina ya mke na mme nyumbani ni tatizo jingine linalosababisha wafanyabiashara kuwa na kauli mbaya kwa wateja wao kwa kuwa hasira wanaipeleka wenye biashara.
"Leo unafanya biashara ukiwa na hasira ya nyumbani na unajikuta unashidwa kuogea na wateja vizuri na kumpa majibu yasiliridhisha juu ya bidhaa/huduma unayouza," alisisitiza.
Waumini wa Kanisa hilo wakifuatilia mahubiri kutoka kwa Askofu David Mabushi
Muumini wa Kanisa hilo, akisoma neno kutoka kwenye Biblia Takatifu
Waumini wakifuatilia neno
Mama Mchungaji wa Kanisa hilo, Suzana Mabushi akitoa neno kwa waumini wa kanisa hilo
Waumini wakifuatilia mafundisho juu ya lugha za biashara
Waumini wa kanisa la IEAGT wakisikiliza kwa umakini mafundisho juu ya umuhimu wa matumizi ya lugha sahihi za biashara
Muumini wa Kanisa hilo akifanya maombi
Waumini wakifanya maombi ya kuombea biashara zao