Koletha Mwita ambaye ameshinda ubunge katika kura za maoni kupitia Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Shinyanga
Suzy Luhende, Shinyanga
ZOEZI la upigaji kura za maoni kupata mwakilishi wa ubunge Viti Maalum kupitia Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga limemalizika, ambapo Koletha Mwita amekuwa mshindi wa mchakato huo baada ya kupata 19 akifuatiwa na Sinzo Mgeja aliyepata kura 7 na Salome Peter kura moja.
Uchaguzi huo umefanyika leo Agosti 2, 2020 katika ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga ukihudhuriwa na wajumbe wapiga kura 27 na wagombea wakiwa watatu, ambapo mshindi huyo anatoka wilaya ya Kahama.
Mchakato huo ulisimamiwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko ambaye amewaomba makada hao wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushirikiana katika kukijenga chama chao.
Kwa upande wake, Mshindi wa kura hizo, Koletha Mwita amewashukuru wajumbe na kusema ataiwakilisha Shinyanga kwenda kwenye mpambano wa kitaifa na kuwaomba wanachama hao wamuombee ili akaweze kushinda.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga, Alhaj Salum Simba amesema mshindi amepatikana baada ya kuongoza kura hivyo haitakiwi kufanya sherehe kwa walioshinda kwani hizo ni kura za maoni tu majina yote yanapelekwa Taifa.
"Jumuia ya Wazazi ndiyo jumuiya yenye uhai ndio inayobeba majukumu, hivyo ni vizuri kushirikiana na chama kukipatia ushindi katika uchaguzi mkuu," amesema.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasitha Mboneko ambaye ndiye msimamizi wa uchaguzi huo akizungumza na wajumbe pamoja na watia nia
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga, Salum Simba akizungumza baada ya kumaliza uchaguzi wa wabunge viti maalumu kupitia jumuiya hiyo.
Mshindi wa pili wa kura za maoni, Sinzo Mgeja akizungumza na wajumbe wakati wa zoezi la kuomba kura
Mshindi wa tatu, Salome Peter.
Wajumbe wa Jumuiya Wazazi mkoa wa Shinyanga wakisubiri kupiga kura za kumchagua mbunge viti maalum kupitia jumuiya hiyo.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Shinyanga, Masanja Salu akizungumza baada ya kumaliza uchaguzi wa mbunge viti maalum kupitia baraza la wazazi