MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MBOGWE NICODEMUS MAGANGA ACHUKUA FOMU

Mgombea ubunge jimbo la mbogwe kwa tiketi ya (CCM) ndg Nicodemus Maganga akipokea fomu ya kuwania kiti hicho toka kwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo ndg Elias Kayandabila

Picha na  Na Shaban Njia

MBOGWE 

MGOMBEA  wa Jimbo la Mbogwe Mkoani Geita Nicodemus Maganga leo tarehe 21 August amechukua fomu ya uteuzi wa kugombea jimbo hilo kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi(CCM) katika ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo.

Akimkabidhi fomu hiyo, Mkurugenzi wa uchaguzi wa jimbo hilo bwana Elias Kayandabila,amesema kuwa,fomu hizo zinatakiwa kujazwa kikamilifu ndani ya muda uliopangwa na kurejeshwa kwake ifikapo tarehe 25 kabla ya saa kumi kamili jioni.

Msimamizi wa uchaguzi amemtaka mgombea huyo  kuzija kwa uangalifu na umakini mkubwa kwa kuepuka kukosea  na kuongeza  kuwa endapo atakosea hakutakuwa na fomu nyingine za ziada.

“Nakupatia fomu hizi ukazisome na kuzijaza kwa ukamini mkubwa,fomu hizi zipo za aina mbili,zipo za lugha ya Kiswahili na lugha ya kiingrereza na usipoelewa fomu za kiingereza zinamwongozo wa lugha ya Kiswahili unaweza kupitia kabla ya kuijaza”Amesema Kayandabila.

Nae katibu wa (CCM) Wilaya Mbogwe Grace Shindika amesema kuwa,wamechukua jukumu la kumfikisha mgombea katika Ofisi za msimamizi wa uchaguzi kuchukua fomu ya uteuzi wakiwa na barua inayonesha kuchaguliwa kwa Nicodemus Maganga kuwa mgombea wa jimbo hilo.

Hata hivyo Shindika amewataka wachama wa (CCM) na wafuasi wa mgombea huyo  kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki cha mpito na kusubilia kampeni zifunguliwe na kuanza kwa mchakato wa kutafuta kura kutoka kwa madiwani, Mbunge na Rais

Nae Mgombea wa jimbo hilo Nicodemus Maganga akiwa mbele ya ofisi za chama amewahakikishia wanachama na wananchi kuwa atahakikisha anashirikiana na serikali kwa ukaribu zaidi katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Mbogwe.

“Ndugu zangu najua mnanijua kwenye kazi,leo sio siku ya kuongea na nitaongea mengi wakati wa siku ya ufunguzi wa kampeni, na siku hiyo nitawapokea watu niliowaacha chama cha democrasia na maendeleo(CHADEMA) na kujiunga na (CCM)”amesema Maganga.

  Mgombea ubunge Jimbo la Mbogwe Nicodemus Maganga akisaini kitabu cha tume ya taifa ya uchaguzi ikiwa ni kumbukumbu za tume kuwa amechukua tayari fomu za kugombea nafasi hiyo.

 Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Mbogwe ndg Elias Kayandabila akimkabidhi fomu ya kugombea nafasi ya ubunge kutpitia CCM 
 
 Zoezi la Kujaza rejesta ya tume ya uchaguzi likiendelea 
 Zoezi linaendelea kwa mgombea kujaza kitabu hicho 

 Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Mbogwe Elias Kayandabila akiendelea kutoa baadhi ya maelezo na maelekezo  ya uchaguzi mkuu wa 2020 kwa mgombea wa jimbo hilo kupitia CCM 

  Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Mbogwe Nicodemus Maganga akiendelea na zoezi la kuwaonyesha wanachama waliojitokeza kumsindikiza kuchukua fomu namna zinavyofanana 

  wanachama na wapenzi wa CCM jimbo la mbogwe wakifurahia Mgombea ubunge  Nicodemus Maganga  kuchukua fomu 

Mgombea Ubunge jimbo la Mbogwe Nicodemus Maganga akiwashukuru wanachama na wananchi kwa kujitokeza kumsindikiza kwenda kuchukua fomu katika ofisi za Msimamizi wa uchaguzi zilizopo Masumbwe.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464