Waziri wa maji Profesa Makame Mbarawa akiangalia namna mabomba yatakayopeleka Maji Masengwa yanavyounganishwa.
Na Shinyanga Press Club Blog
Waziri
wa Maji Profesa Makame Mbarawa amemuagiza Mkandarasi anayetekeleza mradi wa
maji kutoka Shinyanga hadi kata ya Masengwa kukamilika kabla ya mwezi wa tisa kuisha
ambapo mkataba wake utakamilika.
Profesa Mbarawa
ametoa agizo wakati akikagua mradi huo unaotekelezwa na kampuni ya Emirates builders
ya jijini dar ambapo amesema kuwa umekuwa kero na kuchukua muda mrefu pasi kukamilika na.kumtaka
mkandarasi huyo kukamilisha ili wakazi wa Kata ya Masengwa na vijiji jirani
viweze kunufaika na huduma ya maji safi na salama
“Ninaomba
nikwambie kuwa mradi huu ukamilike kabla ya mwezi septemba kwani wananhi
wamekuwa wakipata adha kubwa ya maji ili hali mradi upo hivyo iwapo utashindwa
kukamilisha kwa wakati tutaleta wahandisi wa wizara watakamilisha na hutapewa
kazi yoyote ndani ya wizara ya maji” amesema Mbarawa .
Aidha waziri
Mbarawa amesema kuwa mradi huo umechukua muda mrefu kukamilka kutokana pamoja
na fedha nyingi zaidi ya shilingi bilioni 3 kwa kusema kuwa utaratibu uliotumika
kuwapata wakandarasi haukuwa sahihi ndo maana umetumia fedha nyingi na kutumia wakandarasi ambapo ungetumia mfumo wa
akaunti ya dharura (force Account) mradi huo ungegharimu
fedha kidogo na muda mfupi.
“Ninaomba
nikwambie mwenyekiti wa chama cha mapinduzi siwezi kujilaumu mimi na ninyi
mlishiriki kwa sababu mlikuwa sehemu ya madiwani mliopitisha mradi huu matokeo
yake ni shida lakini hatutakaki kurudi nyumba kazi imefikia asilimia 84
iliyobaki ni kidogo tumekubaliana kabla ya mwezi wa tisa kuisha mradi uwe
umekamilka,” amesema.
Mkuu wa
wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amesema kuwa kutokana na kauli ya mkandarasi huyo kuwa kabla ya tarehe 27 mwezi wa tisa atakuwa amekamilisha
mradi huo atahakikisha anafutailia kwa ukaribu kuona iwapo mradi umekalimika
kwa viwango vinavyotakiwa.
“Naomba
nikuaidi mheshimiwa waziri mimi na kamati yangu nitaendelea kufuatilia kwa
ukaribu mradi huu na kumisimamia ili kuhakikihsa wakazi wa masengwa na maeneo
ya jirani wanapata maji kwa wakati na kuondoa kero iliyowasumbua kwa muda wa
miaka mingi,” amesema
Awali
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Edward Ngelela amesema
kuwa mradi huo umekuwa ukienda taratibu kwa
takribani miaka 3 na kupelekea wananchi kuhangaika kusaka maji na kushindwa kufanya shughuli za
maendeleo.
“Mheshimiwa
waziri nikuombe utusaidie mradi huu ukamilike kwa wakati ili utusadie hata siye
kujieleza kwa wananchi maana kila tunapoenda kuzungumza nao kilio chao kikubwa
ni maji hawana kingine zaidi ya maji,” alisema.
Hata hivyo
Msimamizi wa mradi wa Shinyanga Masengwa Muhandisi Saidi Msangi toka kampuni ya
Emirates amehaidi kutekeleza agizo la waziri na kusema kuwa kabla ya Septemba
27 mradi huo utakuwa umekamilka'
Aidha Waziri
Mbarawa amekagua miradi inayotekelezwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa
mazingira mjini Shinyanga SHUWASA katika Kata za Ngogwa na Kitwana Halmashauri
ya Mji Kahama na kupongeza hatua ambayo miradi hiyo imefikia kutokana na
usimamizi imara wa Mkurugenzi wa SHUWASA Bi Flaviana Kifizi ikiwemo matumizi
mazuri ya fedha
Akizungumzia
ujenzi wa miradi hiyo Mkurugenzi
mtendaji wa Shuwasa Flaviana Kifizi amesema kuwa wametumia mfumo wa akaunti ya dharura na kuchangia
kujenga miundombinu hiyo kwa gharama nafuu
huku akihaidi kutekeleza kwa wakati
ambapo amemuomba waziri kusaidi kuharakisha fedha za kuchimba mitaro kwa ajili
ya kulaza mabomba kiasi cha zaidi ya shuilingi milioni 80 ambapo waziri mbalawa
amemuhakikihsia kuwa fedha hizo zitafika kiwa wakati ndani ya wiki mbili
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarawa akizungumza na Wakazi wa Masengwa wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo ya maji
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akitoa maelezo kwa Waziri wa Maji wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maji mkoani Shinyanga.
Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Shinyanga Muhandisi Emaely Nkopi akiwa katika ziara ya waziri wa Maji.
Waziri wa Maji akiendelea na ukaguzi wa miradi
Tanki la Ngogwa litakalohudumia zaidi ya wakazi elfu 40
Mojawapo ya Tanki la Maji linalojengwa kijiji cha Kitwana
Mkurugenzi wa Shuwasa Bi Flaviana Kifizi akiznugumza mbele ya waziri wa maji
Waziri wa maji profesa Mbarawa akikagua Tanki la maji Kijiji cha Masengwa
Picha zote na Shinyanga Press Club Blog
Picha zote na Shinyanga Press Club Blog