Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Debora Magiligimba
Na Shinyanga Press Club Blog
Mtoto mwenye
umri wa miaka sita anayeitwa Kulwa Machia amefariki dunia baada ya
kung’atwa na fisi usoni na kujeruhiwa vibaya, wakati akitoka kuchunga mifugo
akirudi nyumbani akiwa na watoto wenzake .
Tukio hilo lilitokea
jana majira ya saa 12:00 jioni katika Kitongoji cha Relini Mtaa wa
Nhelegani Tarafa ya Shinyanga Mjini Manispaa
ya Shinyanga,ambapo fisi huyo alimvamia mtoto huyo na kumng’ata usoni kisha
kutokomea vichakani baada ya kusikia mayowe ya watoto waliokuwa na marehemu.
Kamanda wa
jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Debora Magiligimba amesema matukio ya fisi
kujeruhi na kuwaua watoto walio na umri wa chini ya miaka kumi Mkoani Shinyanga
yamekuwa yakiripotiwa mengi na amewataka wazazi na walezi kuchukuwa tahadhari
hasa kipindi hiki.