MWANDISHI JOSEPHINE CHARLES AZIDI KUUPA SAPOTI MPIRA WA KIKAPU SHINYANGA



Mdhamini wa "PayBack Basketball Bonanza 2020", Josephine Charles akizungumza na wachezaji wa Basketball kutoka Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto kabla ya Mchezo kuanza kati ya Timu ya Warrious na Los Angeles katika uwanja wa KCHS mkoani Shinyanga.

Na Mwandishi wetu, Shinyanga
Mdau wa Michezo nchini Bi. Josephine Charles ambaye ni Mtangazaji na Mwandishi wa Habari kutoka Radio Faraja fm Stereo 91.3 ya mkoani Shinyanga amekabidhi mipira miwili kwa wachezaji wa mpira wa kikapu (Basketball) wanaosoma katika Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto kilichopo katika Manispaa ya Shinyanga.

Josephine amekabidhi mipira hiyo katika uwanja wa mchezo wa kikapu Hospitali ya Kolandoto wakati wachezaji hao walipoandaa mchezo mwingine uliopewa jina la PayBack Basketball Bonanza 2020 ambapo yeye ndiyo alikuwa Mdhamini wa Bonanza hilo.

“Natumai mtakuwa watu wa kujituma, fanyeni sana mazoezi kwa lengo la kucheza Basketball kwa ngazi zote ikiwemo kiwilaya,Mkoa,Kanda na kitaifa,nategemea ninyi mtakuwa sehemu ya kuleta mashindano makubwa ya mchezo wa kikapu ili kupendwa na wengi,naahidi nitaendelea kushirikiana nanyi kupitia taaluma yangu ili kila mchezaji wa timu hii afikie malengo aliyojiwekea kupitia mchezo huu.”Alisema Josephine.

Timu zilizoshiriki kucheza katika mchezo wa "PayBack Basketball Bonanza 2020" Ni Warrious na Los Angeles ambapo Warrious waliibabua Los Angeles vikapu 62 kwa 47.

Kwa upande wake Said Ndwela ambaye alikuwa mwamuzi wa Mechi hiyo aliyeongea kwa niaba ya Captain mkuu wa timu hizo,amesema kuwa mchezo huo ulikuwa mzuri na wachezaji wameonesha uwezo mkubwa ambapo kulikuwa na wingi wa vikapu vya point tatu, wakati huo mchezaji wa timu ya Warriors John Magere ameongoza kwa kufunga Vikapu vingi.

“Mchezo wa leo ulikuwa hot sana na Ulikuwa mzuri kuutazama hata kwa mpita njia ila pia wachezaji walikuwa na spirit japo uliandaliwa kwa muda mfupi,” Alisema Ndwela.

Ndwela ameeleza tofauti ya bonanza lililopita na hili ambapo amesema kuwa mchezo huu wa Payback Bonanza 2020 ulikuwa na magoli mengi kuliko mchezo uliopita na wachezaji wamecheza kwa uwezo mkubwa.

Aidha ameishukuru Radio Faraja fm kupitia udhamini wa mwandishi wa habari na mtangazaji wake Josephine Charles kwa kudhamini mipira miwili itakayowasaidia katika mchezo huo.

“Josephine ametufanyia kitu kikubwa kwani tulikuwa na mipira mitatu ila yeye ametuongezea mipira miwili kwakweli ni kitu kikubwa sana na tunamshukuru sana na tunaomba azidi kututafutia wadhamini ili tuweze fikisha mchezo huu mbali katika mkoa wetu wa Shinyanga,” Aliongeza Ndwela.

"PayBack Basketball Bonanza 2020" ni sehemu ya kufanya kumbukumbu ya bonanza la Basketball Bonanza 2020 lililofanyika Julai 25 2020 katika uwanja wa Michezo uliopo jirani na Hospitali ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga ambapo timu ya Hard Target iliibuka kidedea kwa kupata alama 19 wakati Los Angeles walipata alama 17.

Tazama picha hapa chini.

Mdhamini wa Mchezo wa Payback Basketball Bonanza 2020 Bi. Josephine Charles akikabidhi Mipira aliowapa Wachezaji wa mpira wa Kikapu Kolandoto - Shinyanga.
Wachezaji wa Mchezo wa Kikapu(Basketball) wakiwa wamejipanga kwenye mstari wakimsikiliza mdhamini wao Josephine Charles.
Mmoja wa wachezaji wa Mpira wa Kikapu Big Lucas akiwa ameshika mpira mmojawapo waliopewa na mdhamini wa "PayBack Basketball Bonanza 2020" .
Wachezaji wa Mchezo wa Kikapu wakiwa na mdhamini wao katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wa "PayBack Basketball Bonanza 2020" kuanza.
Wachezaji wa Mchezo wa Kikapu wakiwa na mdhamini wao katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wa "PayBack Basketball Bonanza 2020" kuanza.
Wachezaji wa Mchezo wa Kikapu wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wa "PayBack Basketball Bonanza 2020" kuanza.
Mmoja wa Wachezaji wa Timu ya Warrious iliyoibuka na ushindi katika mchezo wa "PayBack Basketball Bonanza 2020" ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kolandoto Dr. Zephania Msunza akiwa katika pozi la picha na mipira waliyopewa na Mdhamini wao Josephine Charles.
Wachezaji wa Timu ya Warrious wakiwa wanajadiliana baada ya Mzunguko wa kwanza wa mechi hiyo kuisha.
Wachezaji wa Timu ya Los Angeles wakiwa wamemaliza kujadiliana baada ya Mzunguko wa kwanza wa mechi hiyo kuisha.
Wachezaji wa timu zote wakiendelea na mchezo wa "PayBack Basketball Bonanza 2020" .
Wachezaji wa timu zote wakiendelea na mchezo wa "PayBack Basketball Bonanza 2020" .
Wachezaji wa timu zote wakiendelea na mchezo wa "PayBack Basketball Bonanza 2020" .
Baadhi ya Wachezaji wakiwa nje ya uwanja kuutazama mpira wa kikapu.
Wachezaji wa timu zote wakiendelea na mchezo wa "PayBack Basketball Bonanza 2020" .
Picha zote na Samir Salum.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464