SPC YAWAKUMBUSHA WAANDISHI WA HABARI MAADILI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU


Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga (SPC), Greyson Kakuru (Katikati) akizungumza jana na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wilayani Kahama kuwakumbusha juu ya weledi na kufuata sheria kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020.


Na Salvatory Ntandu, Kahama
Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) imewataka waandishi wa habari mkoani humo kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia maadili ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanaepuka upendeleo na kutumika na wanasiasa katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu ili kuepuka kuingia katika migogoro isiyokuwa na tija.

Agizo hilo limetolewa Agosti 29, 2020 na Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Greyson Kakuru katika kikao kazi cha siku mmoja na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wilayani Kahama kilichokuwa na lengo la kuwakumbusha umuhimu wa kuzingatia maadili katika utendaji kazi wao.

Alisema kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea katika Uchaguzi mkuu waandishi wa habari wanapaswa kuwa makini zaidi kwa kuandika habari ambazo haziegemei upande wowote ili jamii iendelee kuwaamini katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

“SPC tumeamua tuje tuwakumbushe mapema ili kila mmoja wetu awe makini na asijikute anaingia matatani kwa kuvunja sheria,wakati huu epukeni kuandika habari zinaoegemea upande mmoja ni hatari kwa usalama wa waandishi wa habari,” alisema Kakuru.

Naye Katibu Mtendaji wa SPC, Ali Lityawi alisema kuwa ipo haja ya waandishi wa habari mkoani humo kuhakikisha waangalia usalama wao pindi wanapokuwa kazini husuasani wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao ya kila siku hususani katika mikutano ya Kampeni.

“Suala la usalama ni muhimu kwenu hakikisheni kila mnapokwenda kutekeleza majukumu yenu ya kila siku mnaangalia suala hili,shirianeni na vyama vyote vya siasa katika uchaguzi huu ili wananchi waweze kujua sera za za wagombea nafasi za uongozi mwaka huu zilizopo katika ilani za vyama vyao,” alisema.

Neema Sawaka ni Mwandishi wa habari wa Gazeti la Nipashe,  alisema kuwa kuna umuhimu kwa viongozi wa SPC kufanya uhakiki upya wa waandishi wa habari mkoani humo ili kuwabaini baadhi ya watu wanaovamia fani ya uandishi huku wakijua wazi kuwa si wana taaluma.

Kwa upande wake Ndalike Said Sonda Mwandishi wa habari wa redio Kahama Fm aliwaomba waandhishi wa habari mkoani humo kuwa na umoja na kupendana sambamba na kuacha kusemana vibaya kwa wadau wa habari.

“Tusisemane vibaya kwa wadau wetu,tusemane sisi kwa sisi kwenye vikao kazi vyetu,tusiruhusu wasiokuwa na taaluma kujua madhaifu yetu hii itasaidia kutuweka pamoja katika vipindi vya raha na shida,” alisema Sonda
Baadhi ya waandishi wa habari wilaya ya Kahama wakiwasikiliza viongozi wa (SPC)Mwenyekiti,Greyson Kakuru na Ali Lityawi katika kikao kazi cha siku mmoja.
Katibu Mtendaji SPC, Ali Lityawi akizungumza wakati wa kikao hicho
Waandishi wa habari wakifuatilia kwa umakini hoja kutoka kwa viongozi wao wakati wa kikao kilichowakutanisha jana mjini Kahama
Mwanahabari, Paul Kayanda akifuatilia hoja
 Waandishi wa habari wilayani Kahama wakiendelea kusikiliza mada kutoka kwa viongozi wao
Mwenyekiti wa SPC, Greyson Kakuru (kushoto) na Katibu Mtendaji, Ali Lityawi wakiwasikiliza waandishi wa habari
 Kikao kikiendelea
Majadiliano na uwasilishaji wa maoni vikiendelea wakati wa kikao hicho
Mwandishi wa habari Shaban Njia (kushoto) akichangia hoja
 Kikao kikiendelea
 Viongozi wa SPC wakisikiliza hoja kutoka kwa waandishi wa habari wilayani Kahama katika kikao kilichowakutanisha jana Agosti 29, 2020






Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464