Sehemu ya wananchi wakiangalia Treni mara baada ya kuwasili kwenye Stesheni ya Treni Jijini Arusha ikiwa ni safari ya kwanza baada ya miaka 34 iliyopita kusimama kwa usafiri huo jijini hapa
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi akiongea na Wananchi mara baada ya treni hiyo ya mizigo ikiwa na mabehewa 10 yenye tano 400 kuwasili katika stesheni ya Arusha mapema leo saa tano ikiwa ni safari ya majaribio kabla ya usafiri huo kuanza mwezi huu mwishoni.
Wananchi waliofika kuipokea Treni ya mizigo ya majaribio kwenye hafla ya mapokezi leo jijini Arusha kama walivyokutwa na kamera ya matukio jijini Arusha wakiilaki treni hiyo ikiwasili kwenye Stesheni ya Railway iliyopo Krokoni Kata ya Levolosi jijini Arusha.
Wananchi wakifuatlia hotuba ya Katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Arusha Mwita Zakaria kwenye hafla ya mapokezi ya Treni ya mizgo iliyowasili leo ikiwa ni safari yake ya kwanza baada ya miaka 34 kupita na kuanza tena kutoka huduma mwishoni mwa mwezi huu.
Sehemu ya Mabehewa kumi ya Treni hiyo ya mizigo kama yalivyokutwa na kamera ya matukio jijini Arusha mapema leo katika Stesheni ya Reli iliyopo eneo la Krokoni kata ya Levolosi jijini Arusha
Baadhi ya wananchi wakipata fursa ya kupiga picha na usafiri huo wa Treni ikiwa ni sehemu ya hafla hiyo mara baada ya kuwasili katika stesheni ya reli iliyopo kata ya Levolosi jijini Arusha
Umati wa wananchi na wakazi wa jiji la Arusha waliojitokeza kwenye hafla ya kuwasili kwa treni ya mizigo iliyowasili kwa mara ya kwanza baada ya kitambo kirefu kusimama kwa usafiri huo takribani miaka 34 iliyopita usafiri huo utaanza rasmi mwishoni mwa mwezi huu.
Na
Ahmed Mahmoud Arusha
MAMIA
ya wananchi jijini Arusha wamejitokeza kwa wingi kwenye hafla ya mapokezi ya
Treni ya mizigo ya majaribio iliyowasili ikitokea Dar es salaam na mabehewa
kumi ya Saruji yenye tani 400 na kupokelewa na Mkuu wa wilaya ya Arusha.
Akizindua
hafla hiyo ya mapokezi ,mkuu wa wilaya ya Arusha, Kenani Kihongosi, amewaomba
wananchi kuhakikisha wanailinda na kuitunza miundo mibinu ya reli ili iweze
kudumu na kuwahudumia wananchi .
Ametoa
wito kwa wafanyabiashara kuitumia treni hiyo ya mizigo kusafirishia bidhaa zao
na hivyo kuwapa unafuu wa bei ya bidhaa na kuboresha maisha ya wananchi kama
lilivyo lengo la serikali ya awamu ya Tano kuinua maisha ya watanzania.
Alisema
kuwa ujio wa treni hiyo ya Mizigo ni mwanzo wa treni nyingine ikiwemo treni ya
Abiria itakayosaidia kusafirisha na kushuka kwa bei za bidhaa ikiwemo saruji na
usafiri wa Abiria kwa bei ya 18,000 badala ya elfu 30,000 hadi 35,000 kwa
usafiri wa mabasi.
Aidha
alisema kuwa treni moja itakuwa inapakia tani zaidi ya mia nane za Mizigo sawa
na malori 80 na hivyo kusaidia kuokoa uharibifu wa barabara unaosababishwa na
wingi wa malori ya Mizigo
"Wananchi
lindeni na kutunza miundombinu ya Reli ili isihujumiwe na kuturudisha katika
zama za kale jambo ambalo tunatakiwa tuliona na kutoa taarifa kwa haraka katika
kudhibiti matukio kama hayo"alisema Mkuu huyo
Awali
mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro aliyewasili na treni hiyo kutokea kituo
cha Usariver wilayani Arumeru, hadi jijini Arusha alisema kwa mara ya kwanza
treni hiyo ya mizigo inatambulishwa rasmi kwa wananchi na huo ni mwanzo wa
safari ya maendeleo na kuashiria kupokelewa kwa treni ya abiria ambayo itaanza
mwishoni mwa mwezi huu wa Augosti 2020.
Alisema
serikali ya Chama cha Mapinduzi inayoongozwa na daktari John Magufuli,
inatekeleza Ilani ya uchaguzi kwa vitendo na sio maneno na wananchi ni
mashahidi.
Muro,
amewaomba wafanyabiashara kuituma fursa hiyo ya uwepo wa treni hiyo kusafirisha
bidhaa za viwandani kutoka mikoa mbalimbali kuipeleka mkoani Arusha kutoka na
kwenda mikoa mingine.
Akitoa
salamu zake ,Katibu wa Chama cha Mapinduzi,wilaya ya Arusha, Denis Mwita,
amesema ujio wa treni hiyo ni kurahisisha huduma ya usafirishaji wa
mizigo na kuwapunguzia gharama za mizigo na usafirishaji wananchi.
Alisema
sasa Chama cha Mapinduzi kimefikia mwishoni mwa utekelezaji wa Ilani ya
uchaguzi ya mwaka 2015-2020 ambayo imetekelezwa kwa vitendo na wananchi ni
mashahidi kwa maendeleo yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitano ya awamu
ya kwanza ya rais Magufuli.
Katibu
mwita, alisema mkoa wa Arusha, una viwanda vingi ikiwemo vya mabati na chuma
lakini ni mkoa ambao hauna kiwanda cha Saruji hivyo treni hiyo itatumika
kusafirishia pia Saruji kutoka kwenye mikoa mingine inakozalishwa na kuileta
Arusha hivyo kupunguza gharama za bei za bidhaa na kuwataka wananchi kuendelea
kukiamini Chama cha Mapinduzi na serikali yake.
Aliwaambia
wananchi kwamba hawana cha kumlipa rais Magufuli, kutokana na aliyoyafanya
hivyo wahakikishe wanamlipa kwa kumpatia kura za kutosha kwenye uchaguzi mkuu
utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.
Baadhi
ya wananchi waliokuwepo kwenye hafla hiyo wameishukuru serikali ya awamu ya
tano kwa kuwasogezea huduma hiyo ya usafiri na kuwapunguzia gharama za nauli
kutoka kiasi cha 30.000 hadi Elfu kumi na nane
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464