TVMC YAKUTANA NA VIONGOZI WA MTAKUWWA KUPATA TAARIFA ZA MATUKIO UKATILI WA KIJINSIA SHINYANGA

Mkurugenzi Mtendaji Shirika la TVMC,Musa Jonas Ngangala.
***
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wajumbe wa Kamati za Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wametakiwa kuongeza ubunifu zaidi katika kufuatilia taarifa za vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto ili kutokomeza vitendo hivyo katika jamii.


Hayo yamesemwa leo Ijumaa Agosti 7,2020 na Afisa Tawala wilaya ya Shinyanga, Beda Kamara kwenye kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA kutoka kata saba za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kilicholenga kujadili namna ya kuratibu utoaji rufaa za huduma kwa wahanga wa matukio ya ukatili wa kijinsia.

Kikao hicho kilichoandaliwa na shirika la The Voice of Marginalized Community (TVMC) pia kililenga kujadili namna ya Kamati za MTAKUWWA ngazi ya kata kufanya kazi kwa kushirikiana na taasisi zingine zinazotoa huduma za jamii sambamba na kuifanya jamii kumiliki na kuendeleza MTAKUWWA.

Akifungua kikao hicho, Afisa Tawala huyo wa wilaya ya Shinyanga, aliyemwakilisha Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko alisema ni vyema Wajumbe wa kamati za MTAKUWWA wakaongeza ubunifu kuwafikia walengwa wakiwemo watoto ili kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

“Wajumbe wa Kamati za MTAKUWWA tuongeze mbinu za kutafuta taarifa kwani kuna vitendo vya ukatili havionekani kwa haraka kama ilivyo m imba lakini kuna ukatili hauonekani lakini unaumiza. Kuna familia nyingi zinakutana na ukatili wa kiuchumi. Hebu tuone namna ya kupata taarifa za kutosha ili kupata mbinu za kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto”,aliongeza Beda.

Aliwashauri wajumbe hao wa MTAKUWWA kukutana na viongozi wa vitongoji ili kupata taarifa mbalimbali za masuala ya ukatili wa kijinsia na kutumia mabonanza ya michezo ili kuibua vipaji na kuibua hisia na changamoto zinazowakabili watoto.

Katika hatua nyingine Beda alisema suala la utetezi wa haki za wanawake na watoto ni la kila mmoja katika jamii hivyo ni vyema kila mtu achukue hatua pale anapoona kuna vitendo vya ukatili vinafanyika.

Kwa Upande wake, Mkurugenzi wa Shirika la TVMC, Musa Jonas Ngangala alisema shirika lake limeendelea kutoa mafunzo kwa wajumbe wa kamati za MTAKUWWA katika kata saba za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ambazo ni Samuye, Usanda, Tinde, Nsalala, Didia, Masengwa na Ilola ambako TVMC inatekeleza Mradi wa kupinga ukatili wa kijinsia kwa ufadhili wa shirika la Foundation For Civil Society.

“Kikao hiki cha leo ni mwendelezo wa Shirika la TVMC kuendesha majadiliano na kamati za MTAKUWWA kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia ili kuhakikisha kamati hizi zifanye kazi kwa ufanisi zaidi. Tumeenda kwenye kata 7 za halmashauri ya Shinyanga na tuna mpango wa kuzifikia kata zingine”,alisema Ngangala.

Kaimu Afisa Ustawi wa Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Aisha Omari alisema hali ya wazazi na walezi kutowajibika katika malezi na makuzi ni miongoni mwa sababu zinazochangia uwepo wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.

Aidha alieleza kuwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga imeendelea kutoa elimu ya masuala ya malezi na makuzi,jinsia na kuwezesha wananchi kiuchumi kupitia vikundi vya akina na mama,vijana na watu wenye ulemavu ili kujikwamua kiuchumi.

Mkuu wa Kituo cha Polisi Shinyanga Mjini, Grace Salia aliwataka wananchi kuacha tabia ya kuficha matukio ya vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto huku akiwahamasisha kujitokeza kutoa ushahidi kwenye kesi zinazohusu ukatili ili kukomesha vitendo hivyo katika jamii.

Nao washiriki wa kikao hicho walisema uwepo wa klabu za wanafunzi shuleni zimekuwa msaada mkubwa katika upatikanaji wa taarifa za vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ambapo watoto wenyewe wamekuwa mstari wa mbele kutoa taarifa.

“Kamati za MTAKUWWA zinafanya kazi nzuri na ufuatiliaji umekuwa mzuri na hizi klabu za watoto shuleni zimekuwa msaada mkubwa kwani watoto wenyewe sasa wanatoa taarifa za matukio ya ukatili”,alisema Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Usanda, Halima Tendega.

Kikao hicho kimekutanisha pamoja viongozi wa Kamati za MTAKUWWA ngazi ya kata, Watendaji wa kata na viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga akiwemo Mwanasheria,Afisa Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii, Mganga Mkuu,Hakimu,Polisi, Maafisa Elimu na maafisa kutoka shirika la TVMC ambapo wakati wa kikao hicho wajumbe wa kila kata walitengeneza Mpango kazi wa kutekeleza MTAKUWWA.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI


Afisa Tawala wilaya ya Shinyanga, Kamara Beda akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko kwenye kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA kutoka kata saba za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kilichoandaliwa na shirika la TVMC kwa lengo la kujadili namna ya kuratibu utoaji rufaa za huduma kwa wahanga wa matukio ya ukatili wa kijinsia. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Afisa Tawala wilaya ya Shinyanga, Kamara Beda akisisitiza umuhimu wa kamati za MTAKUWWA kuongeza mbinu zaidi za kutafuta taarifa za matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Shinyanga Mjini,Grace Salia akifuatiwa na Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga,  Janeth Elias.

Afisa Tawala wilaya ya Shinyanga, Kamara Beda akizungumza katika kikao hicho.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la TVMC, Musa Jonas Ngangala akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA kutoka kata saba za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kilichoandaliwa na shirika la TVMC kwa lengo la kujadili namna ya kuratibu utoaji rufaa za huduma kwa wahanga wa matukio ya ukatili wa kijinsia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la TVMC, Musa Jonas Ngangala akifafanua namna shirika la TVMC linavyoshirikiana na serikali katika kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la TVMC, Musa Jonas Ngangala akiwahamasisha wajumbe wa kamati za MTAKUWWA kuendelea kutoa t
Kaimu Afisa Ustawi wa Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Asha Omari akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA kutoka kata saba za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. Mkuu wa Kituo cha Polisi Shinyanga Mjini, Grace Salia akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA kutoka kata saba za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga,  Janeth Elias akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA.
Washiriki wa kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA kutoka kata saba za halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Kikao kinaendelea. Kikao kinaendelea.
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Didia Felister Jonathan Melli akitoa taarifa ya matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika kata ya Didia.
Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Samuye Ibrahimu Bundo akiwasilisha taarifa kuhusu matukio ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika kata ya Samuye. Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Shinyanga,  Opeyo Sisso akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA. Mwakilishi wa Afisa Elimu Msingi wilaya ya Shinyanga,  Joseph Bihemo akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA. Kaimu Mganga Mkuu halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,  Dkt. Mushi Fidelis akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA. Mwanasheria halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Salehe Hassan akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA. Mwakilishi wa Hakimu mahakama ya Mwanzo Usanda,Judith Mnyasi akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA. Mratibu wa UKIMWI halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Happiness Misael Shao akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA. Afisa Maendeleo ya Jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Edmund Ardon akizungumza katika kikao cha viongozi wa kamati za MTAKUWWA.
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Kikao kinaendelea
Washiriki wa kikao wakiwa ukumbini.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464