Vijana mbalimbali wanaoshiriki mafunzo ya jeshi la akiba eneo la Old Shinyanga manispaa hiyo wakiwa katika gwaride wakati mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko alipokuwa akiangalia ukakamavu wa vijana hao.
Vijana 149 toka Manispaa ya
Shinyanga wamejiunga na mafunzo ya jeshi la akiba ikiwa ni sehemu ya
kuhakikisha wanadumisha amani, umoja na ulinzi wa nchi katika maeneo yao pamoja
na kujiimarisha kiafya .
Akifungua mafunzo hayo Agasti 25 Old Shinyanga, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mh
Jasinta Mboneko amewaasa vijana hao kuyatumia
vema mafunzo hayo ya kijeshi yanayotolewa na
Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuhakikisha wanalinda na kudumisha amani ya
nchi pamoja na kujenga mshikamano na umoja
Mboneko amesema kuwa mafunzo hayo ambayo kwa sasa
yamefikisha wiki 7 toka kuanza kwake huku
yakitarajia kuchukua miezi minne ambapo amewataka kuwa na nidhamu wakati wote wa
mafunzo na kuacha kusua kusua kwenye mafunzo.
“Kwa hiyo hakikisheni mnahudhuria mafunzo kila siku lakini
nidhamu iwe ya hali ya juu mpo kwenye mafunzo tunatizama vitu kuna
mnatakavyojifunza darasani na vingine
huku na kila siku nitakuwa napewa taarifa juu ya mafunzo haya kwa hiyo kikubwa
ni kuzingatia na kushika maelekezo
mnayopewa na wakufunzi wenu”amesema Mboneko
Dc Mboneko ameongeza kuwa kwa sasa nchi inaelekea kwenye
uchaguzi mkuu ambapo suala la amani linapaswa kudumishwa ambapo amewaasa kuendlea kutunza nidhamu na
utulivu pamoja na kutoa taarifa za hali
ya uvunjifu wa amani kwenye maeneo wanakotoka
“Kikubwa ni kuhakikisha kwamba maeneo yetu tunakotoka na
kusihi mnakuwa na ninyi ni jicho la serikali na hapa nimeambiwa mko 149
nategemea mmalize wote kwa hiyo niwatahadhirishe msijiingize kwenye
vikundi vya kuhatarisha amani mkono wa
sheria utachukua nafasi yake”ameongeza Mboneko
Naye Mkuu wa mafunzo hayo Kanali Prosper Masawe toka base
ya Shinyanga amesema kuwa jukumu la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ni
kutoa mafunzo kwa lengo la kusaidia
ulinzi kwenye maeneo wanayotoka pamoja na kuimarisha ulinzi wa nchi hususani
nchi inapoingia kwenye vita huwa
tunawatumia katika mapigano.
“Tunawasihi wale Vijana
ambao wako mtaani asijali umri wala elimu kama hajapata mafunzo ya
ulinzi wa nchi yake ni vizuri aje kwenye mafunzo haya ya Jeshi la akiba ambayo
tunatumia miezi minne anakuwa tayari ameelewa kwa hiyo hii ni hatua ya nne
watakwenda hadi hatua ya kwanza”amesema Kanali Masawe
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakiwemo Vijana
ambao ni watumishi wa serikali toka Manispaa ya Shinyanga wamesema kuwa jukumu
la ulinzi wa nchi ni la kila mtanzania hivyo mafunzo hayo yatawasaidia katika
kupamabana na vitendo vya uharifu kwenye maeneo yao
Ezra Majerenga ni Afisa Maliasili na Mazingira Manispaa ya Shinyanga anayeshiriki kwenyemafunzo hayo amesema kuwa katika kuimarisha ulinzi
wa rasimali za nchi lazima uwe na utayari na ukakamvu wa mwili.
“Ili uweze kuwa mlinzi mzuri wa rasilimali za nchi
unastahili kuwamkakavu na unahitaji mbinu za medani kwa maana ya kujua wapi
ambapo maliasili zinatumka vibaya na mifumo ya kuhakiisha kwamba unazilinda kwa
kusimamia sheria na taratibu zilizopo” amesema Ezra
Ufunguzi
huo umeambatana na upigaji wa Shabaha kwa askari hao wa Jeshi la akiba,viongozi
wa serikali wakiongozwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko ikiwa ni
sehemu ya utekelezaji wa uimarishaji wa suala la ulinzi wa nchi.
Baadhi ya Vijana wanaoshiriki mafunzo ya jeshi la akiba Manispaa ya Shinyanga wakiwa wamekaa kumsikiliza mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo hayo mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mh Jasinta Mboneko.
Mshauri wa Mgambo wilaya ya Shinyanga Ford Mwakasege (wa Kwanza) kulia akiwa ameketi pamoja na Mkuu wa mafunzo hayo Kanali Prosper Masawe na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko wakifuatilia mazoezi ya upigaji Shabaha kwa vijana wa jeshi la akiba.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiwa tayari kwa ajili ya kuanza zoezi la upigaji shabaha eneo la Old Shinyanga
DC Mboneko akilenga Shabaha wakati wa zoezi la kupiga shabaha
Afisa Tawala wa Wilaya ya Shinyanga Bw Beda Vedastus akilenga Shabaha wakati wa zoezi la upigaji shabaha
Washiriki wa kulenga shabaha wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kulenga shabaha
Mazoezi ya upigaji shabaha yakiendelea
Baada ya kupiga shabaha wanafunzi wakiwa wameziba masikio yao
Mwandishi na Mtangazaji wa kituo cha kijamii cha mjini Shinyanga Bw Isack Eddo akiwa ameziba masikio baada kuhitimisha kulenga shabaha
Zoezi likiendelea la kulenga na kupiga Shabaha
Afisa Tarafa ya Old Shinyanga naye akilenga Shabaha
Afisa toka ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga akifurahia zoezi la upigaji Shabaha
Afisa Uhamiaji wilaya ya Shinyanga Bw Mwanawima akijiandaa kupiga Shabaha
Mwandishi na Mtangazaji wa kituo cha kijamii cha mjini Shinyanga Bw Isack Eddo akiwa akilenga Shabaha
Mwandishi na Mtangazaji wa kituo cha kijamii cha mjini Shinyanga Bw Isack Eddo akiwa eneo la shabaha kuona iwapo amepata hata moja
Baadhi ya vijana wanaoshirikimafunzo ya jeshi la akiba (Mgambo) wakiwa katika Gwaride la pamoja
Vijana wakiwa wameketi pamoja wakisikiliza ujumbe wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga wakati wa ufunguzi wa mafunzo.
Zoezi la Upigaji na ulengaji wa Shabaha likiendea
Bw Masunga Mchanga ambaye ni dereva wa mkuu wa wilaya ya Shinyanga akilenga shabaha
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiwachangamsha vijana hao kwa kuimba nyimb za uzalendo
Mkuu wa wilaya akiendelea na mazoezi kwa vitendo
Wa Kwanza kulia ni Mkuu wa mafunzo ya jeshi la akiba Kanali Prosper Masawe akimkaribisha Mkuu wa wilaya pamoja na kamati yake katika kushuhudia namna vijana wanavyoshiriki mafunzo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza na waandishi wa habari juu ya umuhimu wa vijana kujiunga na mafunzo ya jeshi la akiba.
Kanali Prosper Maswe toka base ya Shinyanga ambaye ni mkuu wa mafunzo ya jeshi la akiba akitoa maelezo ya mafunzo hayo yatakayofanyika kwa muda wa miezi minne
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464