VITUO 80,155 KUTUMIKA KUPIGIA KURA UCHAGUZI MKUU 2020


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu  ya Mpiga kura (NEC) Bi Giveness Aswile akizungumza na washiriki wa mafunzo ya uchaguzi.
 
Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) imesema kuwa vituo  elfu themanini na Mia moja hamsini na tano (80,155) nchi nzima vitatumika katika zoezi zima la upigaji wa kura za kumchagua Rais, Wabunge na madiwani kwenye uchaguzi mkuu wa October 28,mwaka huu.

Takwimu hizo zimeelezwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu  ya Mpiga kura NEC Bi Giveness Aswile wakati Akizungumza kwenye ufungaji wa  mafunzo kwa waratibu wa mikoa ya Simiyu na Shinyanga,wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi huo yaliyofanyika kwa siku tatu  Mjini Shinyanga.
Aswile amesema kuwa mwaka huu idadi wa wapiga kura imeongeza kutoka watu zaidi ya milioni 23.161  mwaka 2015 hadi kufikia  milioni 29 .188 waliojiandikisha kushiriki katika uchaguzi huo.
Ameongeza kuwa  jumla ya kata ya elfu tatu mia tisa hamsini na sita zinatarajiwa kufanya zoezi la upigaji kura sambamba na majimbo 264 ambapo Tanzania bara  ina majimbo 214  na Zanizbar majimbo 50.


 Wasimamizi na Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kutoka mkoa wa simiyu wakiendelea kufuatilia mahusia ya Kaimu Mkurugenzi wa idara ya habari na elimu kwa mliga kura.

Wasimamizi na Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kutoka mkoa wa Shinyanga wakiendelea kufuatilia mahusia ya Kaimu Mkurugenzi wa idara ya habari na elimu kwa mpiga kura.









Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464