Pongezi
hizo zimetolewa leo (03.08.2020) na Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Waziri
Mkuu( Uwekezaji ) Angellah Kairuki wakati alipohutubia wananchi wa
Simiyu kwenye maonesho ya Nanenane ikiwa ni siku maalum ya kuhamasisha
ushirika.
Amesema
hatua hiyo ya wizara itawezesha wanaushirika ambapo ni wakulima, wavuvi
na wafugaji kunufaika na kazi zao ndani ya ushirika .
“
Ninawapongeza sana Wizara kwa hatua mliyochukua ya kuvifuta vyama vya
ushirika 2,539 kwa sababu ya kutofanya kazi iliyokusudiwa.” alisema
Waziri Kairuki.
Waziri
Kairuki alisema katika kipindi cha 2018/2019 jumla ya viwanda 75
vimeanzishwa na vyama vya ushirika vinavyochata alizeti,
chikichi,kutengeneza samani za majumbani,kuchakata pamba na mazao ya
nafaka pamoja na usindikaji wa maziwa.
“Viwanda
vinavyomilikiwa na vyama vya ushirika vimeongezeka kutoka viwanda 133
mwaka 2018 hadi kufikia viwanda 208 mwaka 2019” alisema Waziri Kairuki.