Wachezaji wa timu zilizoshiriki kucheza mechi ya Kirafiki ya Mpira wa Miguu kati ya Wacheza Mpira wa Kikapu (Basketball) na wachezaji wa mpira wa Miguu (Football) wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mtanange huo kuanza katika uwanja wa Mpira wa Miguu wa Shule ya Msingi Kolandoto Mkoani Shinyanga.
Na Shinyanga Press Club Blog
Katika kuadhimisha sikukuu ya Wakulima (Nane Nane) mwaka 2020, wachezaji wa Mpira wa Miguu na wachezaji wa mpira wa Kikapu (Basketball) kutoka Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto na baadhi ya Wafanyakazi wa Hospitali ya Kolandoto mkoani Shinyanga, wamecheza mechi ya kirafiki ya mpira wa Miguu katika uwanja wa Shule ya Msingi Kolandoto.
Mechi hiyo ilianza kuchezwa majira ya saa kumi na moja jioni na kumalizika saa moja usiku, baada ya Dakika 90 kuisha timu zote mbili zilikiwa na sare ya bao moja kwa moja.
Awali kipindi cha kwanza cha mchezo huo kiliisha kwa sare ya bila bila,ambapo katika kipindi cha pili dakika ya 50 wacheza mpira wa miguu(footballers) walipata goli la kwanza lililofungwa na Ibrahimu Makongoro na katika dakika ya 86 ya mchezo huo wacheza mpira wa kikapu (Basketballers) wakalipa deni kwa kusawazisha bao hilo lililofungwa na John Magere.
Baada ya dakika 90 kukamilika wakaelekea katika mikwaju ya Penalti ili kumpata mshindi wa mechi hiyo, hivyo wacheza mpira wa Kikapu(Basketballers) wakaibuka na ushindi wa penalti 4-2.
Tazama picha hapa chini.
Baadhi ya Wachezaji wa Mpira wa Kikapu walioshiriki mchezo wa Kirafiki wa Mpira wa Miguu wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo kuanza.
Wachezaji wa Timu zote mbili zilizoshiriki kucheza mechi ya Kirafiki ya Mpira wa Miguu kati ya Wacheza Mpira wa Kikapu(Basketball) na wachezaji wa mpira wa Miguu(Football) wakiwa katika picha ya Pamoja kabla ya mtanange huo kuanza katika uwanja wa Mpira wa Miguu wa Shule ya Msingi Kolandoto mkoani Shinyanga.