Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mh Jasinta Mboneko akisikiliza maelezo toka kwa Mkurugenzi wa Kashwasa Muhandisi Joshua Mgeyekwa juu ya utekelezaji wa mradi huo wa maji toka Solwa hadi mwakitolyo.
Wakazi zaidi ya elfu kumi na Nne wa Kata ya Mwakitolyo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
wanatarajia kuondokana na adha ya upatikanaji wa maji baada ya mradi mkubwa wa maji
toka ziwa kuanza kutekelezwa chini ya mamlaka ya maji safi na usafi wa
mazingira Kahama Shinyanga Kashwasa.
Akizungumzia utekelezaji wa mradi huo Mkurugenzi wa Kashwasa Muhandisi Joshua Mgeyekwa amesema
kuwa zoezi linaloendelea kwa sasa ni ulazaji wa mabomba ya chuma ambayo
yatapeleka maji kwenye tanki kubwa lilioko Mwakitolyo ili kuwezesha utoaji wa
huduma ya maji kwa wananchi.
Muhandisi Mugeyekwa
amesema kuwa mradi huo umepitiwa na kufanyiwa upya usanifu kwa ushirikiano kati ya Ruwasa na
Kashwasa baada ya mradi wa awali
uliokuwa ukisimamiwa na halmashauri ya wilaya ya shinyanga kushindwa kufikisha
maji kama ilivyokusudiwa.
“Baada ya usanifu tumeweza kubadilisha aina ya mabomba kwa kutoa ya awali mabayo yalikuwa ya Plastiki na kuweka mabomba ya chuma yenye uwezo wa kuimili
msukumo mkubwa wa maji yaani (Presha ya
maji) inyaofikia zaidi ya Mita 400 PN 40 ambapo tunachukilia maji pale Solwa na
kupeleka kwenye tanki ambalo tayari lilishajengwa awali lenye ujazo wa Mita 90
na urefu wa hili bomba ni Kilomita 20.6”
Mugeyekwa amesema kuwa tayari wamepokea mabomba yenye
kufikia kilomita 14 ambapo wanasubiria bomba zilizosalia pamoja na vifaa vya
kuungia huku akibainisha kuwa mradi huo utakapokamilika utahudumia wakazi wa
mwakitolyo, mawemiru na sehemu za jirani kwa wananchi wapatao elfu kumi
nne na mia sita(14600)
“Mpaka sasa hivi ujenzi umefikia asilimia 60 na
tulitegemea tujenge mradi huu kwa siku
90 yaani miezi mitatu lakini sasa hivi
tumetumia siku 45 lakini ndani ya mwezi mmoja au zaidi tutakuwa
tumemaliza”
William Msabi ni fundi
sanifu kutoka kashwasa amesema kuwa
zoezi la uchimbaji wa mtaro huo lilianza
tarehe 16 mwezi wa sita na tarkibani kilmita 17 zimechimbwa huku kilomita 14 zikiwa tayari zimelazwa bomba
huku akieleza kuwa katika utekelezaji wa mradi huo wamekumbana na changamoto
mbalimbali ikiwemo miamba pamoja na udongo ambao umekuwa ukiwatatiza.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Shinyanga amesema kuwa
miradi mingi ya maji inayotekelezwa na
wakandarasi imekuwa ikisua sua pamoja na
kuchukua muda mrefu na kushindwa kutoa huduma kwa jamii kwa wakati.
“Matumaini makubwa ya wananchi wa kata ya mwakitolyo ni kuona kuwa wanapata maji na
ndicho kilio chao kikubwa kwa hiyo nami nimekuja
kujionea kwamba kazi hii ipo kwenye hatua gani ukizingatia kwamba eneo hili
lina changamoto kubwa ya maji hasa ukianzia mwezi wa 12 hadi wa 4 kulikuwa kumejaa maji hapa na kushindwa
kutekelezeka kwa mardi hata wananchi walikuwa wakisafiri kwa mitumbi hata
barabara zilikuwa zimekatika”
Mboneko amesema kuwa serikali kupitia kwa waziri wa Maji Profesa Makame
Mbarawa imehaidi kuleta fedha kwa ajili ya kumalizia mradi huo na kusema kuwa
mategemeo makubwa ni kukakamilika kabla ya mvua kuanza kunyesha ili wakazi wa
Mwakitolyo waweze.
“Niwapongeze wananchi na wakazi wote wa Mwakitolyo na kata jirani kwa kuendelea kutunza
miundombinu hii ya maji kulinda mabomba haya pia kufanya kazi ya kuchimba
mitaro kwa kweli ninawashukuru sana waendelee kutoa ushirikiano na kulinda na
kutunza miundombinu hii”
Mradi huo unatekelezwa na Mamlaka ya maji safi na usafi wa
mazingira Kahama Shinyanga (KASHWASA) na Wakala wa maji vijijini(RUWASA) kwa gharama ya shilingi bilioni 2 milioni 298
na laki 7 na elfu 51 mia 343
(2.398,751,343) ambapo awali uligharimu
shilingi bilioni 1.4.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Shinyanga wakiendelea kukagua na kuangalia maungio ya maji eneo la solwa ambapo
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama viongozi wa kashwasa na ruwasa wakitembelea eneo ambalo mradi wa maji utaanzia kuelekea mwakitolyo.
wajumbe wa kamati ya ulinzi,watendaji wa kashwasa na ruwasa wakiangalia namna ambavyo mabomba ya chuma yanavyounganishwa chini ni mafundi wa mabomba kutoka kashwasa pamoja na wananchi wakishirikiana kulaza mabomba
Shughuli za kuunganisha Mabomba zikiendelea eneo la Mwakitolyo
Zoezi la kulaza mabomba linaendelea ili kuhakikisha wakazi wa Mwakitolyo wanapata huduma ya maji safi na salama
Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Kashwasa Muhandisi Joshua Mgeyekwa akifuatiwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga wakiteta jambo wakati zoezi la ulazaji na uunganishaji wa mabomba ukiendelea.
Mafundi wakiendelea na zoezi la kuunganisha mabomba ya chuma.
Hili ni eneo la Mwakitolyo ambalo huwa linajaa maji wakati wa msimu wa mvua kwa mbali ni mwoneko wa njia ya bomba la maji linaloendelea kulazwa.
Wajumbe wakiendelea na kukagua mradi huo unaotekelezwa na Kashwasa kwa ushirikiano na Ruwasa
zoezi la kuunganisha mabomba likiendelea chini ya usimamizi wa mafundi toka kashwasa pamoja na wananchi ili kusogeza huduma ya Maji karibu ikiwa ni mwelekeo wa serikali wa kumtua ndoo mwanamke.
baadhi ya Mabomba yakiwa eneo la kuunganishwa
Tayari mabomba yameunganishwa na kulazwa ndani ya mtaro yakisubiri kufukiwa
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464