WASICHANA SITA WENYE MIAKA 10-14 HUAVYA MIMBA KILA SIKU BRAZIRI


Hatua ya kumtoa mimba mtoto wa miaka 10 wiki hii, imezua mjadala mkali Brazil, ambapo suala la uavyaji mimba linakumbwa na mgawanyiko mkubwa.
Lakini Melania Amorim, daktari ambaye amekuwa akiwasaidia waathiriwa wa unyanyasaji wa kijinsia kwa miaka 30, ameiambia BBC kuwa visa kama hivyo vinaendelea kuongezeka na kuelezea kwanini kutoa mimba ndio nji asalama kwa wasichana hao kuliko kujifungua
Melania Amorim alikuwa anaanza taaluma yake daktari bingwa wa wanawake aliposhuhudia kisa cha kwanza cha mimba za utotoni nchini Brazil.
Ilikuwa kisa cha msichana aliye na miaka 13 ambaye alikuwa amebakwa wakati mama yake alipokuwa akifanya kazi za ndani.
Alikuwa amepelekwa hospitali katika eneo la kaskazini -magharibi mwa Brazil ili akatolewe mimba - lakini hakuna daktari yeyote aliyekuwa zamu ambaye alitaka kumfanyia huduma hiyo.
"Mamake msichana huyo alikuwa mfanyakazi wa ndani na alikuwa amemuacha nje kuota jua. Alipata ujauzito baada ya kushambuliwa," Dkt Amorim aliambia BBC.
"Hospitalini, hakuna mtu aliyetaka kumhudumia, kila mmoja alisema anapinga utoaji mimba."
"Nilikuwa mdogo lakini nilikubali kumhudumia. Niliamini kuwa kufanya hivyo ni kuokoa maisha ya mtoto na kwamba ilikuwa haki yake kama mhasiriwa wa ubakaji," daktari alisema, kwa sauti ya masikitiko.
Dkt Amorim amefanya kazi ya kuwahudumia watoto na kushughulikia masuala ya mimba za utotoni kwa zaidi ya miaka 30, hususan wasichana waliopata ujauzito kutokana na ubakaji.
Takwimu za unyanyasaji wa kijinsia ni za kushangaza: kwa mujibu wa data iliyokusanywa na shirika lisilokuwa la kiserikali la Public Safety Forum ambalo linajishughulisha usalama wa umma, wasichana wanne walio na umri wa chini ya miaka 13 wanabakwa kila baada ya saa moja kila siku.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464