WASIMAMIZI WA UCHAGUZI MKUU SHINYANGA NA SIMIYU WAPEWA MAFUNZO

 Wasimamizi wa uchaguzi mkuu kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu wakila kiapo cha kusimamia haki kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Na Marco Maduhu -Shinyanga

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi mkuu ngazi za majimbo katika mkoa wa Shinyanga na Simiyu, ili kufanikisha uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu, wa kuchagua madiwani, wabunge na Rais ufanyike kwa haki na huru.

Akifungua mafunzo hayo leo mjini Shinyanga Kamishina wa Tume ya taifa ya uchaguzi Balozi Omari Mapuli, ambayo yatachukua muda wa siku tatu, alisema Nec inaendesha mafunzo kwa wasimamizi hao wa uchaguzi pamoja na wasaidizi wao, wakiwamo na maofisa ugavi, ili kuwajengea uwezo namna ya kusimamia zoezi zima la uchaguzi mkuu.

Amesema wameendesha mafunzo hayo ili kufanikisha zoezi zima la uchaguzi mkuu linafanyika kwa ufanisi na kuondoa malalamiko kwa vyama vya siasa, na umalizike kwa amani bila ya kutokea vurugu zozote zile, kwa kuzingatia katiba ya nchi, sheria za uchaguzi, maadili na kanuni zake.

“Tume ya taifa ya uchaguzi tunatoa mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya majimbo na wasaidizi wao kutoka Shinyanga na Simiyu, lengo ni kuhakikisha uchaguzi mkuu ambao utafanyika Oktoba 28 mwaka huu, unafanyika kwa haki na huru na kumalizika kwa amani,” amesema Mapuli.

“Mnatakiwa kutambua kuwa mmeaminiwa na tume, na kuteuliwa kufanya zoezi hili la kusimamia uchaguzi, jambo la muhimu ni kujiamini, kujitambua, pamoja na kuongozwa na katiba ya nchi, sheria ya uchaguzi, maadili na kanuni zake wakati wa kutekeleza majukumu yenu ili kuhakikisha uchaguzi una malizika salama,” ameongeza.

Kwa upande wake Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga, Fabiani Kamoga, amesema mafunzo hayo yanatija kubwa kwa wasimamizi hao wa uchaguzi ngazi ya majimbo, ambapo pia watayashusha ngazi ya Kata, ili uchaguzi mkuu ufanyike kwa haki na huru, bila kutokea malalamiko yoyote yale kwa vyama vya kisiasa.


TAZAMA PICHA HAPA CHINI



Kamishina wa Tume ya taifa ya uchaguzi Balozi Omari Mapuli, akifungua mafunzo ya wasimamizi wa uchaguzi mkuu mkoa wa Shinyanga na Simiyu.


Mratibu wa uchaguzi mkoani Shinyanga Fabiani Kamoga akizungumzia faida za mafunzo hayo.

Wasimamizi wa uchaguzi mkuu wakiwa kwenye mafunzo.

Wasimamizi wa uchaguzi mkuu wakiwa kwenye mafunzo.

Wasimamizi wa uchaguzi mkuu wakiwa kwenye mafunzo.

Wasimamizi wa uchaguzi mkuu wakiwa kwenye mafunzo.

Wasimamizi wa uchaguzi mkuu wakiwa kwenye mafunzo.

Wasimamizi wa uchaguzi mkuu wakiwa kwenye mafunzo.

Wasimamizi wa uchaguzi mkuu wakiwa kwenye mafunzo.

Wasimamizi wa uchaguzi mkuu wakila Kiapo.

Picha Zote na Marco Maduhu- Shinyanga








Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464