Shirika lisilo la kiserikali la AGAPE ACP ambalo linatetea haki za wanawake na watoto mkoani Shinyanga, kwa kushirikiana na Serikali limetoa elimu kwa akina mama wa Kata ya Didia halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, namna ya kuzingatia Lishe bora kwa watoto wao, ili kukabiliana na magonjwa mbalimbali ikiwamo udumavu, pamoja kinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.
Elimu hiyo imetolewa leo Ijumaa Septemba 11,2020 katika eneo la Didia na kukutanisha wanawake 40 kutoka kwenye vijijini vitano vya kata hiyo, kila kijiji kikiwa na akina mama wanne wenye watoto walio na umri chini ya miaka sita, ili wakawe mabalozi kwa wenzao, ambapo pia wamefundishwa namna ya kulima viazi Lishe pamoja na matumizi yake.
Akizungumza kwenye mafunzo hayo mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE ACP John Myola, amesema wametoa mafunzo hayo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wao wa uboreshaji wa Lishe bora kwa watoto, ili kuwapatia kinga imara ya mwili ambayo itawafanya kujikinga na magonjwa mbalimbali yatokanayo na upungufu wa kinga mwilini.
Amesema mradi huo ulianza utekelezaji wake Julai mwaka huu na utakoma Juni 2021, ambao unatekelezwa kwenye kata hiyo ya Didia kwa ufadhili wa Shirika la Firelight, ambao walengwa wakuu wa mradi huo ni watoto walio chini ya umri wa miaka sita, ili kuimarisha kinga ya miili yao.
“Tumetoa mafunzo kwa akina mama wa kata hii ya Didia namna ya kuzingatia Lishe bora kwa watoto wao, pamoja na kuwafundisha namna ya kulima viazi Lishe na matumizi yake, ili kuimarisha kinga ya mwili kwa watoto, ambao ndio waathirika wakubwa wa magonjwa mbalimbali ambapo hata virusi vya Corona vilikuwa vikishambulia zaidi watoto na wazee,”amesema Myola.
“Elimu ambayo imetolewa leo kwa akina mama hawa 40 kutoka kwa Afisa kilimo, Lishe na wadau wa Lishe, itakwenda kuwa mbegu kwa wenzao ambapo kila mmoja anatakiwa aunde kikundi cha wanawake 10, ili wawe na mashamba darasa ya viazi Lishe, kitendo ambacho kitasaidia kuondoa tatizo la udumavu kwa watoto,”ameongeza.
Naye Afisa Lishe wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Mankiligo Said, akitoa elimu hiyo aliwataka akina mama wawe wananyonyesha watoto wao ndani ya miaka miwili ili kuwajengea kinga ya mwili, pamoja na kupika chakula kwa kuzingatia makundi matano ya chakula.
Aidha ametaja hali Lishe katika halmashauri hiyo ya wilaya ya Shinyanga, udumavu ni asilimia 33, ambapo lengo ni kupunguza hali hiyo hadi kufikia asilimia 27 ifikapo mwaka 2025.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Deusi Mhoja, akimwakilisha mkurungezi wa halmashauri hiyo Hoja Mahiba, amelipongeza Shirika hilo la Agape kwa kuendelea kushirikiana na Serikali kutatua changamoto mbalimbali, likiwamo suala la Lishe na ukatili dhidi ya watoto wadogo.
Pia amewataka akina mama hao wakaunde vikundi vya ujasiriamali, ili wapate mkopo wa halmashauri, ambao utawawezesha kulima mashamba makubwa ya viazi Lishe, na kuwaingizia kipato na kukuza uchumi wa familia zao, licha ya kutumia kwa matumizi ya chakula.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI