SHIRIKA LA SNV LAWAPIGA TAFU WANAONYONYA MAJI TAKA MANISPAA YA SHINYANGA


 Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira Manispaa ya Shinyanga, Kuchibanda Snatus (wa tatu kulia) akikabidhi Shaban Abdalah kutoka Kampuni ya Shaban Investment vifaa kinga vilivyotolewa na Shirika la SNV kwa wamiliki wa magari ya huduma ya kunyonya maji taka ‘Tope Kinyesi’ katika halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ili kulinda afya za wafanyakazi. Wa kwanza kushoto ni Afisa kutoka SNV Issack Msumba,  wa tatu kushoto ni Meneja Ufundi kutoka SHUWASA, Mhandisi Yusuph Katopola. Wa kwanza kulia ni  Mshauri wa Miradi ya Usafi na Mazingira kutoka shirika la SNV, Sauli Mwandosya akifuatiwa na Afisa Afya na Mazingira Msaidizi  Idara ya Mazingira Manispaa ya Shinyanga, Ramadhan Hamimu. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira Manispaa ya Shinyanga, Kuchibanda Snatus (wa tatu kulia) akikabidhi Shaban Abdalah kutoka Kampuni ya Shaban Investment vifaa kinga vilivyotolewa na Shirika la SNV kwa wamiliki wa magari ya huduma ya kunyonya maji taka ‘Tope Kinyesi’ katika halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ili kulinda afya za wafanyakazi.
Kushoto ni Shaban Abdalah kutoka Kampuni ya Shaban Investment na Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira Manispaa ya Shinyanga, Kuchibanda Snatus (kulia) wakisaini makubaliano ya kutumia vifaa kinga,kibali cha kunyonya tope kinyesi na ya matumizi ya GPS. Katikati ni Meneja Ufundi kutoka SHUWASA, Mhandisi Yusuph Katopola.
Muoneno wa vifaa kinga vilivyotolewa na shirika la SNV kwa kila mmiliki wa magari yanayotoa huduma ya kunyonya majitaka ambavyo ni mabuti,miwani maalumu, gloves, barakoa ngumu ‘Industrial masks’, nguo maalumu,kofia ngumu, viaksi mwanga. Pichani ni vifaa kinga vilivyogawiwa kwa mtoa huduma mmoja.
Mshauri wa Miradi ya Usafi na Mazingira kutoka shirika la SNV, Sauli Mwandosya akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa kinga kwa wamiliki wa magari ya huduma ya kunyonya maji taka ‘Tope Kinyesi’ katika halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ili kulinda afya za wafanyakazi.
Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira Manispaa ya Shinyanga, Kuchibanda Snatus akizungumza wakati wa kupokea na kukabidhi vifaa kinga vilivyotolewa na shirika la SNV kwa wamiliki wa magari ya huduma ya kunyonya maji taka ‘Tope Kinyesi’ katika halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ili kulinda afya za wafanyakazi.
Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira Manispaa ya Shinyanga, Kuchibanda Snatus akiwakumbusha wamiliki wa magari ya huduma ya kunyonya maji taka ‘Tope Kinyesi’ kuhakikisha wafanyakazi wao wanatumia vifaa kinga,wanafanya ukaguzi wa mara kwa mara wa vifaa na wananunua vifaa vingine pale vilivyopo vinapochakaa.
Meneja Ufundi kutoka SHUWASA, Mhandisi Yusuph Katopola akiwasihi watoa huduma za kunyonya maji taka kutumia vifaa kinga walivyopatiwa na shirika la SNV kwa malengo yaliyokusudiwa huku akiwaasa kuwa na utamaduni wa kutumia vifaa kinga ili kulinda afya zao.
Afisa afya na Mazingira Msaidizi  Idara ya Mazingira Manispaa ya Shinyanga, Ramadhan Hamimu akitoa elimu ya namna ya kutumia vifaa kinga kwa wawakilishi wa Manispaa ya Shinyanga, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) na SNV na wamiliki na wafanyakazi kwenye magari ya utoaji huduma za maji taka.
Kulia ni Afisa kutoka SNV Issack Msumba akimvalisha vifaa kinga Clement Mzia kutoka Kampuni ya OK Investment namna ya kuvaa vifaa kinga wakati wa kutoa huduma ya kunyonya majitaka 'Tope kinyesi'. Kushoto ni Afisa afya na Mazingira Msaidizi  Idara ya Mazingira Manispaa ya Shinyanga, Ramadhan Hamimu.
Kulia ni Afisa kutoka SNV Issack Msumba akitoa elimu namna ya kuvaa vifaa kinga wakati  Clement Mzia kutoka Kampuni ya OK Investment akionesha kwa vitendo namna ya kuvaa vifaa kinga wakati wa kutoa huduma ya kunyonya majitaka 'Tope kinyesi'.
 Muonekano wa Clement Mzia kutoka Kampuni ya OK Investment baada ya kuvaa vifaa kinga tayari kwa kutoa huduma ya kunyonya majitaka 'Tope kinyesi'.
Muonekano wa Clement Mzia kutoka Kampuni ya OK Investment baada ya kuvaa vifaa kinga tayari kwa kutoa huduma ya kunyonya majitaka 'Tope kinyesi'.
Wawakilishi wa Manispaa ya Shinyanga, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) na SNV na wamiliki na wafanyakazi kwenye magari ya utoaji huduma za maji taka wakiwa katika picha ya pamoja.
Wawakilishi wa Manispaa ya Shinyanga, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) na SNV na wamiliki na wafanyakazi kwenye magari ya utoaji huduma za maji taka wakiwa katika picha ya pamoja.



Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Shirika la SNV (Netherland Development Organization) limekabidhi vifaa kinga vyenye thamani ya shilingi milioni 2 kwa wamiliki wa magari ya huduma ya kunyonya maji taka ‘Tope Kinyesi’ katika halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ili kulinda afya za wafanyakazi.

Zoezi la kukabidhi vifaa kinga vilivyonunuliwa na shirika la SNV umefanyika leo Ijumaa Septemba 11,2020 katika ukumbi wa Vigimark Hotel Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na wawakilishi wa Manispaa ya Shinyanga, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) na SNV na wamiliki na wafanyakazi kwenye magari ya utoaji huduma za maji taka.

Akizungumza wakati wa kugawa vifaa kinga, Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira Manispaa ya Shinyanga, Kuchibanda Snatus alilishukuru shirika la SNV kwa kuungana na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na SHUWASA kuleta maendeleo na kuboresha afya ya jamii hasa kwa watoa huduma ya unyonyaji wa maji taka.

Alisema lengo la kugawa vifaa hivyo ni kufanya huduma ya unyonyaji maji taka ‘Tope kinyesi’ iwe bora kwa watoa huduma za wanaopewa huduma. 

“Naomba Wamiliki wa magari ya huduma ya kunyonya maji taka tuungane kulinda afya za wafanyakazi wetu kwa kuwa mstari wa mbele kuhimiza matumizi ya vifaa kinga wakati wote”,alisema Snatus.

“Vifaa hivi vimenunuliwa na shirika la SNV kulingana na utafiti uliofanyika baada ya kugundua changamoto mbalimbali zilizokuwa zinawakabili watoa huduma ikiwemo walengwa kutovaa vifaa kinga hata kama wanavyo ama kutokuwa navyo,upatikanaji wa vifaa kinga na hata waliokuwa navyo vilikuwa havina ubora unaotakiwa au vimechakaa”,alieleza Snatus.

Snatus aliwakumbusha wamiliki wa magari ya huduma ya kunyonya maji taka ‘Tope Kinyesi’ kuhakikisha wafanyakazi wao wanatumia vifaa kinga,wanafanya ukaguzi wa mara kwa mara wa vifaa na wananunua vifaa vingine pale vilivyopo vinapochakaa.

Kwa upande wake, Meneja Ufundi kutoka SHUWASA, Mhandisi Yusuph Katopola aliwataka watoa huduma za kunyonya maji taka kutumia vifaa kinga walivyopatiwa kwa malengo yaliyokusudiwa huku akiwaasa kuwa na utamaduni wa kutumia vifaa kinga ili kulinda afya zao.

Mshauri wa Miradi ya Usafi na Mazingira kutoka shirika la SNV, Sauli Mwandosya aliyataja Makampuni ya wamiliki wa magari ya huduma ya kunyonya maji taka waliopatiwa vifaa kinga kuwa ni Shaban Investment, Kweka Investment,OK Investment,Salum Kifaa Donda na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

“Tumekabidhi vifaa kinga vyenye thamani ya takribani shilingi milioni 2 kwa makampuni binafsi matano na halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ambapo kuna magari matano ya Makampuni binafsi na gari moja la Manispaa ya Shinyanga”,alisema Mwandosya.

Alivitaja vifaa kinga vilivyotolewa na shirika la SNV kuwa ni mabuti,miwani maalumu, gloves, barakoa ngumu ‘Industrial masks’, nguo maalumu,kofia ngumu, viaksi mwanga.

Ugawaji wa vifaa kinga umefanyika sanjari na utoaji elimu namna ya kutumia vifaa kinga hivyo pamoja na zoezi la Wadau wa Huduma ya Unyonyaji maji taka ‘Tope Kinyesi’ katika Manispaa ya Shinyanga kusaini makubaliano ya kutumia vifaa kinga,kibali cha kunyonya tope kinyesi na ya matumizi ya GPS.

Nao wamiliki na wafanyakazi wa magari yanayotoa huduma ya kunyonya majitaka walishukuru kwa kupatiwa vifaa na shirika la SNV na kuomba zoezi la kutoa vifaa na elimu liwe endelevu ili kuhakikisha wanalinda afya zao.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464