Mgombea Urais kwa tiketi ya (ADA TADEA) Mh John Shibuda akihutubia wakazi wa Maswa mapema Septemba 27 wakati akizundua kampeni zake kitaifa
Na Shinyanga Press Club Blog
Wakati joto la uchaguzi likizidi kuchukua nafasi kwa wagomea wa nafasi za urais,ubunge na udiwani kupamba moto ambapo wagombea wa nafasi ya urais ni vyama kumi na tano vilipitishwa na tume ya taifa kwa wagombea wake kupeperusha bendera.
Mgombea Urais kupitia chama cha ADA TADEA, John Shibuda amesema kuwa chama hicho hakina uadui na chama chochote cha kisiasa nchini badala yake maadui wakubwa wa chama cha ADA TADEA ni Ujinga, Umaskini na Maradhi huku vita kuu ya chama hicho ni kuhakikisha utawala bora unapatikana
Shibuda amebainisha hayo hii leo Septemba 27, 2020 wakati akizindua kampeni za chama hicho kitaifa wilayani Maswa Mkoa waSimiyu ambapo amesema kuwa suala la Umaskini,Ujinga na Maradhi bado ni tatizo kubwa nchini.
“Sisi kama chama cha ADA TADEA hatuna tatizo lolote na vyama vingine vya siasa bali tatizo letu kubwa ni mapambano dhidi ya madhira watatu ambao ni ujinga,maradhi na Umaskini na vita ya chama chetu ni kuhakikisha kuwa utawala bora unapatikana”
Amesema kuwa chama iwapo chama hicho kitapata ridhaa ya watanzania kimejipanga kuondoa maadui wakubwa wa ustawi na maendeleo ya jamii ya watanzania ambapo amewaomba watanzania kumpigia kura ili awezea kuongoza dola.
Katika hatua nyingine Shibuda ametaja vipaumbele vinnne vya chama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu ikiwemo suala la utawala wa sheria wakati wote kwa wananchi na watendaji wa umma sambamba na siasa safi
Amesema kuwa atawajibika kwa uwazi,ushirikishwaji, uwajibikaji, ufanisi na uadilifu
Mgombea Ubunge Jimbo la Maswa Magharibi kupitia chama hicho, Lydia Mbuke Bendera amewaomba wakazi wa Maswa kumpigia kura ili aweze kutatua kero ,changamoto na adha mbalimbali ambazo zimeendelea kuwepo ndani ya jimbo hilo kwa kipindi cha miaka mingi .
Amesema kuwa iwapo atachaguliwa suala la kwanza kushughulikia ni changamoto ya kina mama kusafiri umbali mrefu,kero ya miundombinu pamoja na kumtua ndoo mama kichwani ikiwa ni kusogezwa huduma karibu na wananchi.
Shibuda akipokelewa na vijana wa chama hicho kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni za chama cha ADA TADEA kitaifa wilayani Maswa
John Shibuda akiwapungia mkono wananchi baada ya kuwasili uwanjani wilayani Maswa
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha ADA TADEA, John Shibuda akisaini kitabu cha wageni wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho kitaifa mkoani Simiyu
Shibuda akipanda jukwaani kwa ajili ya kuzungumza na wananchi pamoja na wapenzi wa chama chake waliojitokeza kusikiliza sera zake katika uwanja wa Majengo wilayani Maswa
Shibuda akizungumza na wananchi wa wilaya ya Maswa katika uzinduzi wa kampeni za chama cha ADA TADEA
Shibuda akiendelea kuinadi sera na ilani ya chama chake kwa wananchi wa wilaya ya Maswa kwenye uwanja wa Majengo
John Shibuda akiteta jambo na mama yake mzazi kwenye uzinduzi wa kampeni za chama cha ADA TADEA kitaifa wilayani Maswa
Mama mzazi wa John Shibuda akimuombea kura mwanae kwa wananchi wa mkoa wa Simiyu
John Shibuda akiwa amevalishwa mavazi ya asili ya kabila la Kisukuma wakati wa uzinduzi wa kampeni za cama cha ADA TADEA kitaifa zilizofanyika wilayani Maswa mkoa wa Simiyu
John Shibuda akisalimiana na baadhi ya wanafamilia waliofika kumuunga mkono kwenye uzinduzi wa kampeni zake wilayani Maswa
Wananchi wa eneo la Majengo wilayani Maswa mkoa wa Simiyu wakifuatilia kampeni za chama cha ADA TADEA zilizozinduliwa katika eneo hilo
Umati wa wananchi wa maeneo mbalimbali ya wilaya ya Maswa ukiwa tayari kusikiliza sera za chama cha ADA TADEA katika uwanja wa Majengo wilayani humo
Wananchi wakifuatilia kampeni za chama cha ADA TADEA
Mgombea Ubunge Jimbo la Maswa Magharibi kupitia ADA TADEA, Lydia Mbuke Bendera akiomba kura kwa wananchi
Mgombea Ubunge Jimbo la Maswa Mashariki kupitia chama cha ADA TADEA, Mipawa Ndilizu akiomba kura kwa wananchi wakati wa mkutano huo wa kampeni
Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama cha ADA TADEA akiomba kura kwa wananchi waweze kukichagua chama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu
Wananchi wa Jimbo la Maswa Magharibi wakimsikiliza mgombea ubunge wa jimbo hilo, Lydia Bendera
Wananchi wa jimbo la Maswa Magharibi mkoani Simiyu wakiendelea kufuatilia uzinduzi wa kampeni za chama cha ADA TADEA katika uwanja wa Majengo wilayani Maswa