Mkurugenzi wa Airtel Money, Isaack Nchunda akizungumza leo jijini Dar es Salaam baada ya kutangaza kuanza kugawa Tzs 3.6 bilioni kama gawio la faida kwa wateja na mawakala wa Airtel ambao wamekuwa wakitumia huduma hiyo. Airtel imekuwa ikigawa gawio hilo la faida kwa wateja wake wa Airtel Money pamoja na mawakala tangu 2015
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya simu za Mkononi ya Airtel Tanzania kupitia huduma ya Airtel Money leo imetangaza kuanza kugawa Tzs 3.6 bilioni kama gawio la faida kwa wateja ambao wamekuwa wakitumia huduma hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari wakati wa kutangaza hatua hiyo ya kugawa gawio la faida kwa wateja wa Airtel Money .
Mkurugenzi wa Airtel Tanzania Isack Nchunda alisema kuwa faida hiyo itagaiwa kwa wateja wote wa Airtel Money pamoja na mawakala nchini ambao wamekuwa wakitumia huduma za Airtel Money kwa kipindi cha Oktoba 2019 mpaka Machi 2020.
Airtel imekuwa ikigawa gawio hilo la faida kwa wateja wake wa Airtel Money pamoja na mawakala tangu 2015.
Faida hii anaipata mteja yeyote wa Airtel kulingana na kiasi kilichopo kwenye akaunti yake yaani salio la Airtel Money.
Gawio hili la faida limekuwa likitolewa na Airtel tangu mwaka 2015 ambapo hadi leo hii jumla ya bilioni 24 TZS zitakuwa zimegaiwa kwa mgawanyo tofauti tofauti na kuwafikia wateja pamoja na mawakala wote nchini, Nchunda alisema.
Nchunda alisema kuwa mteja anaweza kutumia faida hiyo kwa matumizi mbali mbali ikiwemo kununua bando, muda wa maongezi, kulipia bili kama vile Dawasco, LUKU, Dstv, au mteja anaweza akatoa fedha hizo kwa matumizi ya kawaida au kuwatumia ndugu, jamaa na marafiki.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Beatrice Singano alisema kuwa kila mteja wa Airtel Money pamoja na mawakala watapata faida yao kupitia akaunti zao za Airtel Money kuanzia leo.
“Mawakala wa Airtel Money wote watapokea faida yao kupitia akaunti zao za Airtel Money kama kawaida, hivyo ninawaomba waendelee kutoa huduma bora kwa wateja wote nchini ili tuendelee kupata faida kwa robo ya mwaka inayofuata na wote tufaidike," Alisema Singano
“Airtel Money tumefanya maboresho ya kupanua wigo wa kutoa huduma kila kona ya mji na vijijini ili kutimiza dhamira yetu ya kutoa huduma nafuu na haraka, kupitia Airtel Money Branches kwa sasa tunayomaduka ya Airtel Money branches zaidi ya 1,700 ambayo yanafanya huduma za Airtel Money kupatikana kwa urahisi nchini kote”.
Singano aliongeza kuwa “Airtel Money bado inaendelea kuwa na ubunifu wa huduma za kisasa zaidi ili kuendelea kuleta tija na suluhisho la unafuu zaidi kwa wateja, Ni kwa kupitia Airtel Money pekee ambapo wateja sasa wanaweza kutuma pesa bure kupitia applikesheni ya Airtel Money, mteja wa Airtel anatakiwa kupakua applikesheni hiyo kupitia Play Store au App Store na kuanza kufaidi kutuma pesa bure Airtel kwenda Airtel sasa”.
Huduma ya Airtel Money imeunganisha na huduma za biashara zaidi ya 400 pamoja na benki zaidi ya 30 ambapo mteja anaweza kufanya malipo au miamala akiwa popote pale kwa kutumia simu. Vile vile wateja wanaweza kulipia huduma na bili mbali mbali kama vile TRA, LUKU, malipo ya serikali na zingine nyingi.
Meneja Uhusiano Airtel Tanzania akizungumza leo jijini Dar es Salaam baada ya kutangaza kuanza kugawa Tzs 3.6 bilioni kama gawio la faida kwa wateja na mawakala wa Airtel ambao wamekuwa wakitumia huduma hiyo. Airtel imekuwa ikigawa gawio hilo la faida kwa wateja wake wa Airtel Money pamoja na mawakala tangu 2015