Na Patrick Mabula-Kahama
Mratibu wa Huduma za Afya Uzazi na Mtoto Halmashauri ya Mji Kahama, Carolyne Marcel amewataka akinamama wanapopata ujauzito kuzingatia elimu ya afya wanayopewa na wataalamu wa afya ili waweze kujifungua salama.
Akizungumza katika tamasha la akinamama wanaonyonyesha watoto walio na chini ya miezi sita wa kata ya Mwendakulima la kutoa elimu kuhusu faida ya kumyonyesha mtoto maziwa ya mama pale anapojifungua hadi miezi sita kunavyomsaidia kuwa na afya nzuri ya akili na mwili.
Marcel aliwataka wakinamama wanapopata ujauzito kwanza kuwahi mapema hospitari , kituo cha afya na zahanati na kufaata elimu wanayopewa na wataalamu wa afya na kuacha kufata ushauri wa mitaani unawaosababishia kuweza kupata matatizo wakati wa kujifungua .
Amewataka akinamama kuacha mila na destuli potofu ya kutumia dawa za miti shamba wanapokuwa wajawazito na wanapojifungua wasiwapatie watoto kwa sababu zimekuwa zikiwasababishia matatizo mbalimbali ya kiafya bali wafaate elimu wanayopewa na wataalamu wa afya na wahudumu wa afya ngazi ya jamii.
Balozi wa mradi wa Naweza, Zuwena Mohamed maarufu kwa jina la Shilole alisema suala la akinamama kuwanyonyesha watoto wanapojifungua ni la lazima kama tunavyotakiwa na wataalamu wa afya ili mtoto kumuepusha kuwa na utindio wa ubongo unaotokana na sababu ya kutonyonyeshwa ipasavyo maziwa ya mama.
Akitoa elimu hiyo katika tamasha lililokuwa limeandaliwa na shirika la SHDEPHA+ katika mradi wake wa “ Tulonge Afya Twaweza “ unaohusu kutoa elimu ya afya ya mama na mtoto na umuhimu wa kuwayonyesha watoto maziwa ya mama anapojifungua tu hadi miezi sita kunavyoweza kusaidia kukuwa vizuri kiakili na kimwili.
Kaimu mratibu wa elimu ya afya kwa umma ngazi ya jamii wa halmashauri ya mji wa Kahama , Vestina Mutakyahwa kifudisha elimu ya kunyonyesha watoto alisema mtoto anapozaliwa tu anatakiwa anyonyeshwe maziwa ya mama pekee hadi miezi sita na asipewe rishe ya aina yoyote kunamfanya akue vizuri kiakili na kimwili.
Shirika la SHIDEPHA+ linalotekeleza mradi wa TULONGE AFYA TWAWEZA unaohusu kutoa elimu kwa akinamama wanaonyonyesha watoto kuanzia wanapojifungua hadi miezi sita bila kuwapatia rishe yoyote ili waweze kukua vizuri kiakili na kimwili pamoja na kutoa elimu ya afya ya mama na mtoto na matumizi sahihi ya chadarua katika kupambana na ugonjwa wa maralia.