AWATAKA WAPINZANI KUACHA KUBEZA KAZI ZA MAENDELEO ZILIZOFANYWA NA RAIS

 


Mdau wa maendeleo Jeremiah Jilili na kada wa ccm. 


Suzana Luhende,Shinyanga press club blog

Wakati mchakato wa kampeni za uchaguzi mkuu wa kuchagua madiwani, wabunge na Rais ukiendelea nchini, mdau wa maendeleo mkoani Shinyanga ambaye pia ni kada wa CCM Jeremiah Jilili amesema baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wamekuwa wakibeza na kupotosha mambo mengi na makubwa  yaliyofanywa na serikali ya chama cha Mapinduzi CCM chini ya Dr John Pombe Magufuli.

Akizungumza katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari wa Shinyanga press club blog , amesema miradi mingi  imesimamiwa na Rais wa awamu ya tano John Pombe Magufuli, lakini vyama vya upinzani havijaona kilichofanyika, badala ya kueleza mafanikio makubwa yaliyopatikana katika nchi.

"Kwa kweli mimi nashangazwa Sana na wapinzani hawa kwa kuendelea kubeza kazi zilizofanywa na Rais Magufuli wa awamu ya tano na huku wao wenyewe walikuwa wanapigia debe bungeni, lakini baada ya kutekelezwa hawaoni tena kilichofanyika ukiwasikiliza vizuri unashindwa kuwaelewa wanachotaka ni kipi"anauliza Jilili.

Alisema anasikitika kuona  mgombea urais wa Chadema Tundu Lissu wakati  alipokuja mkoa wa Shinyanga kueleza kuwa serikali haiwajali wachimbaji wadogo jambo ambalo hata wachimbaji wao hawawezi kukubali kutokana na serikali kuwajali na kuwapatia maeneo wachimbaji wadogo.

Wachimbaji wadogo wa madini mkoa wa Shinyanga awamu ya tano imewafanyia mambo mengi makubwa ikiwemo kuwapa leseni za uchimbaji, kuwajengea masoko ya madini,kuweka miundoni wezeshi migodini kama umeme, pamoja na upatikanaji wa watalamu wa madini kwenye maeneo ya migodi jambo ambalo limepunguza ajali migodini.

Jilili anasema awamu ya kwanza ya serikali ya awamu ya tano chini ya Dr. John Pombe Magufuli imefanya mambo makubwa katika sekta zote hapa nchini, zaidi ya yale ambayo yamekuwa yakipigiwa kelele na wapinzani na kuleta usawa kwa watanzania wote bila kujali vipato vyao na imeongeza nidhamu na uwajibikaji kwenye ofisi zote za umma.

" Watanzania nawaomba wakati tunaenda kuchagua tuhakikishe kwamba tunafanya maamuzi kwa busara na si kwa mihemko na ushabiki na kwa kufanya hivyo naamini Dr.John Pombe Magufuli bado tunamwitaji kutufikisha katika nchi ya ahadi ambayo anatakiwa kuendelea kuiandaa"anasema Jilili. 

Amesema wameona akifufua shirika la ndege kwa kuongeza ndege nyingi ambazo zimekuwa chachu ya kukuza utalii, kuongeza mapato kupitia utalii kwa nia ya kuitangaza nchi.

Jilili anawaomba wanashinyanga wasikubali kuyumbishwa na watu  wanaopotosha na huku wao wana uraia wa nchi mbili, hivyo kinachotakiwa ni kumchagua tena Rais Magufuli na kwa sababu yeye ni Rais wa wanyonge na uzalendo wake dhidi ya Taifa la Tanzania na Africa haviwezi kutiliwa shaka hata kidogo, na mataifa mengi wanatamani wangeongozwa na Rais Magufuli kwa sababu ni kiongozi wa mfano. 

Baadhi ya wananchi wa mk0a wa Shinyanga Amina Khamis na David Mandalu wanasema ni kweli Rais Magufuli amefanya Mambo makubwa kwa miaka mitano na imeonekana Ni Rais mwenye msimamo akiona mtu kafanya kinyume ndani ya kazi anaondolewa kwenye nafasi hiyo.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464