Baadhi ya wananchi, wafanyabiashara na wachimbaji wa madini waliofika kwenye maonesho ya tatu ya teknolojia na uwekezaji mkoani Geita waliotembelea banda la Tume ya Madini wakipata ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwenye sekta ya madini.
Na Mwandishi Wetu, Geita
WADAU mbalimbali wameendelea kumiminika katika banda la Tume ya Madini kwenye maonesho ya tatu ya Teknolojia na Uwekezaji yanayoendelea kwenye uwanja wa Bombambili mjini Geita, huku baadhi ya watembeleaji wakiwemo wananchi, wafanyabiashara na wachimbaji wa madini wakiipongeza Wizara ya kwa mabadiliko ya Sheria ya madini
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kufika katika banda hilo wakiuliza maswali na kupata ufafanuzi wa mambo mbalimbali, wamepongeza kazi inayofanywa na Wizara ya Madini na Tume ya Madini katika usimamizi makini wa Sekta hiyo.
Wamesema mabadiliko makubwa ya Sheria ya Madini na kanuni zake yaliyofanywa na Wizara ya Madini yameleta mapinduzi makubwa kwenye Sekta ya Madini kwa kuwa manufaa ya dhahabu yameanza kuonekana katika mkoa wa Geita.
"Geita ya sasa imebadilika sio kama zamani, mji unakua kwa kasi sana kutokana na ongezeko la shughuli za uchimbaji na biashara ya madini," amesema Jackson Peter ambaye ni mchimbaji mdogo wa madini ya Dhahabu katika mkoa wa Geita kwa niaba ya wadau wengine wa madini.
Wadau wa sekta ya madini wakiwa kwenye banda la Tume ya Madini kwenye uwanja wa Bombambili mjini Geita kwa ajili ya kufahamu mambo mbalimbali yanayohusu sekta hiyo
Maofisa kutoka Tume ya Madini wakitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali kwa wadau wa sekta ya madini waliofika kwenye uwanja wa Bombambili mjini Geita kutembelea banda la tume hiyo
Wadau wa sekta ya madini wakiwa wamefurika kwenye banda la Tume ya Madini kupata ufahamu wa mambo mbalimbali
Maofisa wa Tume ya Madini wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa sekta ya madini waliotembelea banda la tume hiyo kwenye maonesho ya madini mkoani Geita
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464