Na Shinyanga Press Club Blog
Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) imeendelea kuvifungia viwanja vya michezo nchini ambavyo vimeonekana kuwa na mapungufu mbalimbali na kutokidhi kutumika kwa michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Baada ya jana Septemba 27, 2020 kuufungia uwanja wa Jamhuri uliopo mkoani Morogoro, sasa vinafika viwanja vinne ambavyo tayari vimekutana na rungu la Bodi ya Ligi na kufungiwa hadi pale vitakapofanya marekebidho na kukidhi matakwa.
Viwanja vilivyofungiwa hadi sasa tangu kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara mnamo Septemba 6, mwaka huu ni Gwambina Stadium uliopo Misungwi, Mabatini unaotumiwa na Ruvu Shooting uliopo mkoani Pwani, Karume uliopo mjini Musoma unaotumiwa na timu ya Biashara United pamoja na uwanja wa Jamhuri Morogoro uliokuwa unatumiwa na Mtibwa Sugar kama uwanja wa nyumbani.
Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro