Kulia ni Mgombea ubunge jimbo la Mbogwe (CCM) Nicoedamas Maganga akiwa ameshikiria Ilani ya chama hicho itakayotekelezwa kwa kipindi cha miaka 5 pembeni yake akiwa ni diwani wa kata ya Lulembela, Lyankando Kadushi kwa pamoja wakionesha ilani itakayotumika.
Salvatory Ntandu- Mbogwe
Chama cha Mapinduzi (CCM)
Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita kimezindua kampeni za Ubunge kwa Jimbo la Mbogwe
kwa lengo la kuomba ridhaa kwa wananchi kumchagua mgombea wake Nicodemas
Maganga katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Akizungumza leo na Wananchi wa
kata ya Lulembela katika Mkutano wa Kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo hilo, Mwenyekiti wa (CCM)
mkoa wa Geita, Alhaj Said Kalidushi amewataka wananchi wa jimbo hilo kuwachagua
wagombea wa chama hicho katika nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani.
Alisema kuwa CCM Mpya
inayoongozwa na Rais wa awamu ya Tano Dk John Pombe Mgufuli imejipanga
kuhakikisha inatatua kero za wananchi kupitia ilani yake ya mwaka 2020-2025
ambayo inakwenda kutekelezwa na wagombea wake na kuwataka wananchi kuwa na
imani na wagombea wa chama hicho.
“Mchagueni Rais Dk John Pombe
Magufuli, Mchagueni Nicodemas Maganga kuwa mbunge wa jimbo la Mbogwe na
wachagueni Madiwani 17 wa kata wa CCM ili wakatekeleza Ilani yetu kwa vitendo, tumedhamiria
kutatua changamoto zinazowakabili wananchi katika sekta za elimu, afya na miundombinu ya
barabara,”alisema Kalidushi.
Kwa upande wake Mgombea ubunge
wa jimbo hilo, Nicodemas Maganga wakati akiomba kura kwa wananchi amesema kuwa
endapo atapewa ridhaa ya kuongoza jimbo hilo atahakikisha anatatua chagamoto
zinazowakabili wananchi hususani katika sekta za afya,elimu,Maji na Miundombinu
ya barabara.
“Katika jimbo hili
kunachangamoto mbalimbali katika sekta ya afya ikiwemo uhaba wa watumishi wa
afya hali ambayo inachangia kuwepo kwa vifo vya
akinamama wajawazito na watoto pindi wanapokwenda kujifungua,”alisema
Maganga.
Aliongeza kuwa atahakikisha
anaisimamia serikali katika ujenzi wa miundombinu ya barabara ambayo bado ni
changamoto katika jimbo hilo ikiwemo Madaraja ili kuwawezesha wananchi kundelea
na shughuli za Uzalishaji Mali bila ya kuwa na kikwazo chochote.
Nae Katibu wa CCM wilaya ya
Mbogwe amewaomba wananchi wa jimbo la hilo kuhakikisha ifikapo tarehe 28 mwezi
wa kumi kuhakakisha wanampigia kura Rais Magufuli,Mbunge wa jimbo hilo Nicodemas Maganga na Madiwani
wote wa chama hicho katika kata zote 17.
Aliongeza kuwa Chama cha
Mpinduzi (CCM) kinasera nzuri ambazo zinalenga kuwakomboa wananchi kwa kuwaboreshea Miundombinu mbalimbali
ambapo kwa miaka mitano iliyopita chini ya Rais Dk John Pombe Magufuli
kimetekeleza miradi mikuwa ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara, umeme,
Maji, Reli na ununuzi wa ndege ambazo zote zinalenga kuhakikisha watanzania
wananufaika nazo.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Alhaj Said Kalidushi akisaini kitabu cha Wageni katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni Jimbo la Mbogwe kushoto ni Katibu wa Chama hicho wilaya Mbogwe, Grace Shindika. |
Mgombea ubunge jimbo la Mbogwe Nicodemas Maganga akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa CCM waliohudhuria katika ufunguzi wa kampeni za Ubunge wa jimbo hilo. |
Baadhi ya wagombea Ubunge wa Mkoa wa Geita wakiteta jambo katika mkutano wa ufunguzi wa Kampeni kwa jimbo la Mbogwe. |
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Geita Alhaj Said Kalidushi akumnadi mgombea Ubunge jimbo la Mbogwe Nicodemas Maganga kwa wananchi. |
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbogwe kwa kipindi cha 2015-2020 Agostino Masele akimwombea kura Mgombea ubunge wa Jimbo la Mbogwe wa jimbo hilo Nicodemas Maganga. |
Baadhi ya Wananchi wanaoliohudhuria katika mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa kampeni wa Jimbo la Mbogwe uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Lulembela. |
Mgombea Ubunge wa jimbo la Mbogwe Nicodemas Magaga akielekea kwenda kutoa zawadi kwa vikundi vya ngoma katika hafla ya uzinduzi wa Kampeni katika jimbo la Mbogwe. |
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbogwe Agostino Masele akiwashukuru wananchi wa jimbo hilo kwa kumpigia kura katika uchaguzi uliopita kulia ni Katibu wa Siasa na uenezi wa mkoa wa Geita, David Azari. |
Vikundi vya sanaa vikitoa burudani |