Na Marco Maduhu - Shinyanga
Serikali mkoani Shinyanga imeipongeza Benki ya CRDB, kwa kuwakopesha wafanyabishara fedha kwa ajili ya kununua zao la Pamba kutoka kwa mkulima kwenye msimu wa kilimo uliopita, ambapo soko la zao hilo liliyumba duniani.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, amebainisha hayo leo, wakati akifungua mafunzo kwa mawakala wa Benki hiyo ya CRDB, namna ya kutoa huduma bora kwa wateja ikiwamo njia ya kidigital, iliyohusisha mawakala 300 kutoka wilaya ya Nzega, Kishapu, halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, na manispaa ya Shinyanga.
Amesema Serikali inatambua mchango mkubwa kwa taasisi za kifedha hapa nchini. ambapo kwenye msimu wa zao la pamba uliopita benki hiyo ya CRDB ili kuwa mkombozi mkubwa kwa kutoa fedha kwa wafanyabiashara, ili kununua pamba ya mkulima ambapo ununuzi wake ulianza kusuasua kutokana na soko la zao hilo kuyumba duniani.
“Benki hii ya CRDB ina mchango mkubwa sana Serikalini, ambapo kwenye msimu wa zao la Pamba mlitushika sana mkono, na salamu hizi zifikisheni kwa Mkurugenzi wenu mkuu wa CRDB (Abdulmajid Nsekela), na Serikali tutaendelea kushirikiana na ninyi,” amesema Telack.
“Pia kupitia mawakala wenu naambiwa wananchi wamelipa kodi zaidi ya Shilingi Bilioni 300 kwa mwaka jana, na mwaka huu hadi sasa wamelipa zaidi ya Bilioni 350, huu ni udhiririsho kuwa benki hii ya CRDB ni kichocheo kikubwa cha maendeleo ya taifa ” ameongeza.
Pia Telack amewataka Mawakala wa Benki hiyo kuwa makini wakati wa utoaji wa huduma zao za kifedha kwa wananchi, hasa katika kipindi hiki ambalo taifa lipo kwenye uchumi wa kati, na kutojiingiza kwenye masuala ya utakatishaji fedha, ambapo mtu akifika kuweka mamilioni ya fedha kwao, wamhoji kwanza amezitoa wapi ili kutoshiriki kwenye makosa hayo.
Aidha amewaonya mawakala hao wasijiingize pia kwenye biashara za ukopeshaji kwa kutoza riba kubwa, ambazo ni kandamizi kwa wananchi wakiwamo na wafanyakazi, na kukamata kadi zao za ATM, NHIF, kutokana na kushindwa kurejesha marejesho, na kuwafanya kuwa na maisha magumu zaidi, kuwa atakaye bainika atashughulikiwa.
Naye meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi inayounda mikoa ya Shinyanga , Tabora, Kigoma, Geita, na wilaya ya Sengerema, Saidi Pamui, amesema wameendesha mafunzo hayo ya utoaji huduma bora kwa mawakala wa benki hiyo, pamoja na kuwa makini hasa katika kipindi hiki ambapo Tanzania imeingia kwenye uchumi wa kati, ili wasijiingize kwenye masuala ya utakatishaji fedha.
Nao baadhi ya mawakala hao akiwamo Jamila Kilangi, amesema mafunzo hayo yatawasaidia kuwa makini wakati wa utoaji huduma kwa wateja wao, na kuepuka matapeli na kutojiingiza kwenye masuala ya utakatishaji fedha bila ya kujua, ili kukwepa mkono wa Serikali pamoja na wao kushuka kiuchumi.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akiendelea kuzungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya mawakala wa benki hiyo.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Saidi Pamui,akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga Luther Mneney, akisistiza mawakala hao kuzingatia mafunzo ambayo wamepewa ili yakawe msaada katika utoaji wao wa huduma kwa wananchi.
Wakala wa benki ya CRDB Jamila Kilangi akielezea namna mafunzo yalivyokuwa msaada katika utoaji wao wa huduma za kifedha kwa wananchi.
Mawakala wa benki ya CRDB wakiwa kwenye mafunzo.
mafunzo yakiendelea.
mafunzo yakiendelea.
mafunzo yakiendelea.
mafunzo yakiendelea.
mafunzo yakiendelea.
mafunzo yakiendelea.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, (katikati) mwenye ushungi kichwani, akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki ya CRDB Pamoja na Mawakala wa benki hiyo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464