Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mh Jasinta Mboneko na kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya wakikagua ujenzi wa Madarasa mawili katika Shule ya Msingi Mwalugoye.
Mapema Septemba 16 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Jasinta Mboneko Amefanya ziara katika baadhi ya Shule za Msingi na Sekondari zilizopokea fedha toka serikalini kwa lengo la
kuongeza miundombinu ya Madarasa na Matundu ya Vyombo Manispaa ya Shinyanga.
amesema kuwa serikali imetoa fedha
zaidi ya Shilingi Milioni 600 kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba vya Madarasa na
matundu ya vyoo kwa lengo la kupunguza adha na kero kwa watoto wa shule
Akiwa shule ya Msingi Mwihando
Kata ya Old Shinyanga Mboneko amekagua ujenzi wa Vyumba viwili vya madarasa
pamoja na matundu ya vyoo ambapo amemtaka fundi anayetekeleza mradi huo
kukamilisha kwa wakati ili kuondoa kero kwa wanafunzi wa shule hiyo
“Ili iwe kwa wote
wanaotekeleza ujenzi wa miundombinu ya Serikali hususani kwa shule zilizopata
fedha hakikisheni mnakamilisha ujenzi huo kwa wakati na ifikapo Septemba 30
miundombinu hii ianze kufanya kazi na
ndiyo lengo la serikali kwenye hili”
Mboneko ameongeza kwa kusema
kuwa uwepo wa miundombinu hiyo utasaidia
wanafunzi wengi kufanya vizuri katika
mitihani yao kutokana na kupunguza adha ya kukaa kwa mrundikano madarasani
pamoja na kutumia matundu machache ya Vyoo ambapo ameendelea kusisitiza suala la
ushirikishawaji wa wananchi kwenye miradi ya maendeleo ili kuisaidia serikali kwani haiwezi tekeleza
majukumu yote
“Naomba niwaambie nyinyi
viongozi wa Serikali za Vijiji na Kamati za Shule waambie wazazi pia washiriki
kwenye miradi hii ya maendeleo kwai tazama serikali imekwisha toa mwanga kwa
kuleta fedha kwa ajili ya ujenzi wa
madarasa na Matundu ya vyoo basi nanyi jitoeni walau kwa darasa moja kwa
sababu hawa ni wetu”
Aidha Mboneko akiwa shule ya Sekondari Old Shinyanga
amekerwa na kitendo cha ujenzi wa Bweni
katika shule hiyo kusimama kwa kile kinachodaiwa kuwa BOQ yake ilikuwa juu kuliko fedha iliyotolewa na Serikali kwa ajili ya Ujenzi huo ambapo serikali muhandisi
alitakiwa kubadili BOQ kulingana na fedha iliyotolewa
Akitoa taarifa ya
kusimama kwa Mradi huo Kaimu Mkurugenzi
wa Manispaa ya Shinyanga Bw John Tesha amesema
kuwa makadirio ya muhandisi wa ujenzi wa manispaa hiyo ilikuwa shilingi milioni
160 ambapo fedha iliyotumwa na serikali ni Shilingi Milioni 80 hali
iliyochangia kushindwa kuendlea hadi pale walipobadili BOQ
“Kuhusiana na Kusimama kwa Ujenzi wa jengo la Bweni kwa
ajili ya wanafunzi wa Shule hii ni tatizo la BOQ kwa hiyo tumekwisha rekebisha
na fundi ataanza nadhani kuanzia muda wowote na litakamilika kwa muda rafiki
licha ya kuwa nje ya mkataba”
Nao baadhi ya Walimu wakuu wa Shule zinazotekeleza miradi
hiyo ya Vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo Manispaa ya Shinyanga wakabainisha utekelezaji
wa miradi hiyo licha ya kukumbana na changamoto ya ukosefu wa Saruji hali iliyokuwa
ikikwamisha miradi kutekelezeka kwa wakati
Anna Alute ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bugoyi A
amesema kuwa ujenzi wa Madarsa umefikia hatua ya kufanya Finishingi ikiwemo
upigaji wa Lipu huku ujenzi wa matundu ya Vyoo ukifikia asilimia 95
“Kwa Upande wetu sisi Bugoyi A tumejitahidi kusimamia fedha
zilizotolewa na Serikali na ningependa kutumia fulsa hii kumshukuru Mheshimiwa
Rais kwa kutukumbuka na muda c mrefu
matumizi yake yatakuwa tayari na kabla ya Septemba 30 tutakuwa tumekamilisha”
Naye Malale Sawaka Mkuu wa Shule ya Sekondari Ngokolo
amesema kuwa wao wamepokea fedha kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba vitatu vya
madarasa pamoja na Matundu ya Vyoo ambapo tayari yako kwenye hatua ya Lipu
“Mpaka sasa zoezi linaloendelea ni upigaji wa Lipu pia
tumeshajenga miundombinu kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalaumu ili
kuwawezesha kupita bila kikwazo kwenye milango
kwa hiyo hatua nzuri tunazidi kuipiga”
Mwarabu Mwimbili
ni Mwenyekiti wa kamati ya Shule Mwalugoye ameeleza kufurahishwa na
hatua iliyochukuliwa na serikali kwa kuhakikisha inatia fedha kwa ajili ya kutatua kero za watoto wa shule ikiwemo
uhaba wa madarasa na upungufu wa matundu ya Vyoo
Kwa upande wake aliyekuwa
naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga John
Kisandu ameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuleta fedha hizo na kuzigawa
kwa shule amabzo zinatekeleza ujenzi wake kwa kutumia mfumo wa fosi akaunti
“Mimi nimefurah kiukweli kuona
mambo mazuri kiasi hiki kwani fedha hzi zingeenda kufanya kazi zingine lakini
zimeletwa huku hivyo sisi tuna jukumu la kuhakikisha miradi inakamilika na
kuleta tija kwa jamii ambapo watoto wetu kukaa kwa msongamano kutapungua”
Mwishooo