Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Biswalo Mganga leo Septemba 06 ,2020 amewafutia Mashtaka washitakiwa 95 waliokuwa katika Gereza la Mkoa wa Geita.
Biswalo amewafutia Mashtaka hayo baada ya
kutembelea na kuzungumza na baadhi ya washtakiwa ndani ya Gereza la Mkoa wa Geita kisha kujionea hali halisi ya uendeshaji wake, ambapo pia Biswalo amekagua na kusikiliza Mahabusu na wafungwa walioko ndani ya Gereza hilo.
Mkurugenzi huyo wa mashtaka nchini(DPP) ametaja sababu mbalimbali zilizopelekea kuwafutia mashtaka ikiwa ni pamoja na wale wenye
makosa madogo,ushahidi kuwa hafifu Wazee na Vijana chini ya umri wa miaka kumi na nane(18) baada ya kuwahoji.
Awali akizungumza na washtakiwa hao Mkurugenzi wa Mashtaka amewataka kuacha kujihusisha na vitendo viovu vitakavyowafanya kuingia tena Gerezani badala yake wakawe mfano bora kwa kuwa raia wema kwa jamii wanayokwenda kuishi nayo.
Katika ziara hiyo ya kutembelea na kukagua gereza hilo mkurugenzi mkuu wa mashtaka nchini Biswalo Mganga ameongozana na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa
Geita.
Mwonekano wa Gerezani la Wilaya ya Geita Mkoani humo lililotembelewa na mkurugenzi wa Mashitaka nchini DPP Biswalo Mganga mapema hii leo Septemba 6,2020
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga akizungumza na maafisa wa jeshi la Magereza,Kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoani Geita kabla ya kutembelea na kukagua Gereza la Wilaya ya Geita
Wajumbe wa kamati ya Usalama pamoja na Maafisa wa magereza wakiendelea kusikiliza ujume wa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP Biswalo Mganga