EMMANUEL NTOBI WA CHADEMA AZINDUA KAMPENI NGOKOLO, AAHIDI KUANZISHA SACCOS YA KATA

Mgombea udiwani Kata ya Ngokolo katika Manispaa ya Shinyanga kupitia Chadema, Emmanuel Ntobi akinadi Sera zake kwa Mwananchi wa Kata hiyo katika uwanja wa Ngokolo Mitumbani leo Septemba 15, 2020.

Na Marco Maduhu -Shinyanga
Mgombea udiwani wa Kata ya Ngokolo katika Manispaa ya Shinyanga kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Emmanuel Ntobi, amenadi sera zake kwa wananchi wa kata hiyo leo Septemba 15, 2020 katika Uwanja wa Ngokolo Mitumbani na kutoa ahadi ya kuboresha sekta ya elimu, afya, kujenga Soko, kituo cha Polisi, barabara, pamoja na kuanzisha Saccos ya Kata ili kuinua wananchi kiuchumi.

Ntobi ametoa ahadi hizo leo wakati akizundua rasmi kampeni zake kwenye Kata hiyo ya Ngokolo, mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Ngokolo mitumbani, na kuhudhuliwa pia na Mgombea ubunge wa Jimbo la Shinyanga mjini kupitia Chadema Salome Makamba.

Amesema ndani ya miaka mitano katika utawala wake alipokuwa diwani wa Kata hiyo ya Ngokolo, kuna vitu vingi ambavyo amevifanya kwa ajili ya maendeleo ya wananchi, na kuomba wampe tena mitano mingine ili kamilishe miradi mingine ambayo alikuwa ameianza pamoja na kuinua wananchi kuichumi kwa kuanzisha Saccos ya Kata.

“Kwenye uongozi wangu nilipokuwa diwani kuna vitu vingi ambavyo nimevifanya ukiwamo ujenzi wa Ghuba, kukarabati shule mbili za msingi Mwadui na Mapinduzi, kujenga kituo cha Polisi mtaa wa majengo kipo kwenye hatua za mwisho, ujenzi wa barabara kiwango cha Lami, na utatuzi wa migogoro,” amesema Ntobi.

“Pia nilitafuta wafadhili kutoka Denmark walinipatia vifaa tiba, vikagawiwa kwenye maeneo mbalimbali ya huduma za afya hapa manispaa, ambapo tena vifaa hivyo vilitumwa lakini mpaka sasa vimezuiliwa bandarini bila ya sababu za msingi,” ameongeza.

Aidha alitaja vipaumbele vyake endepo wananchi wakimchagua tena kuwa diwani wao, atajenga kituo cha afya, kumalizia kituo cha Polisi, kuboresha sekta ya elimu , kujenga Soko, Garden ya kupumzikia wananchi , pamoja na kuanzisha Saccos ya Kata ambayo itasaidia kuinua uchumi wa wananchi.

Katika hatua nyingine alitaja sababu za kufukuzwa mara kwa mara kwenye vikao vya baraza la madiwani la manispaa ya Shinyanga, kuwa inatokana na kupigania masuala ya ufisadi ikiwamo kupinga ungezeko la Tozo kwenye vibanda vinavyomilikiwa na manispaa, nakubainisha hata Rais John Magufuli alilisema alipokuwa Shinyanga.

Alisema kitu kingine ni kupinga kupandishwa wananchi bei ya kuuziwa viwanja na manispaa ya Shinyanga, kutoka Shilingi Laki Tano hadi Milioni 2, na kudai aliundiwa njama za kutolewa nje ya kikao ili bajeti hiyo ipitishwe.

Kwa upande wake mgombea ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini Salome Makamba kupitia chama hicho, amewataka wananchi wa Kata hiyo wasifanye makosa siku ya Oktoba 28, bali wampigie kura Emmanuel Ntobi ili awe diwani pamoja na yeye, na Mgombea urais Tundu Lissu ili wakafanye kazi pamoja ya kuwaletea maendeleo.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mgombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Salome Makamba akizungumza na wananchi wa Kata ya Ngokolo.
Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Shinyanga Khamisi Ngunila, akiomba kura kwa wananchi wa Shinyanga kuwapigia kura wagombea wote wa udiwani kutoka Chadema, Mbunge Salome Makamba pamoja na Rais Tundu Lissu.
Mgombea udiwani Kata ya Ngokolo Chadema, Emmanuel Ntobi, kulia, akimuombea kura kwa wananchi wa Ngokolo Mgombea ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini Salome Makamba.
Awali viongozi wa Chadema, na wafuasi wa chama hicho, wakiwa na mgombea udiwani Kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi.
Wananchi wa Kata ya Ngokolo wakiwa kwenye Kampeni za mgombea udiwani wa Kata hiyo Emmanuel Ntobi wakisikiliza Sera zake.
Wananchi wa Kata ya Ngokolo wakiwa kwenye Kampeni za mgombea udiwani wa Kata hiyo Emmanuel Ntobi wakisikiliza Sera zake.
Wananchi wa Kata ya Ngokolo wakiwa kwenye Kampeni za mgombea udiwani wa Kata hiyo Emmanuel Ntobi wakisikiliza Sera zake.
Wananchi wa Kata ya Ngokolo wakiwa kwenye Kampeni za mgombea udiwani wa Kata hiyo Emmanuel Ntobi wakisikiliza Sera zake.
Wananchi wa Kata ya Ngokolo wakiwa kwenye Kampeni za mgombea udiwani wa Kata hiyo Emmanuel Ntobi wakisikiliza Sera zake.
Mgombea udiwani Kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi, mwenye gwanda, akiwa na Mgombea ubunge Jimbo la Shinyanga mjini Salome Makamba, mara baada ya kumaliza kuzindua Kampeni kwenye Kata hiyo.






















Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464