KATAMBI AAHIDI KUTENGENEZA MTANDAO WA MAJI MWAMALILI

MGOMBEA  ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Patrobas Katambi akinadi sera zake kwa wapiga kura kata ya Mwamalili 

Suzy Luhende.Shinyanga

MGOMBEA  ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi amewaomba wananchi wa kata ya Mwamalili manispaa ya Shinyanga wamchague ili aweze kuwatua ndoo kina mama kwa kuwatengenezea mtandao mkubwa wa maji.

Amesema hayo mapema  leo wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Mwamalili, ambapo amewaomba wananchi wa kata hiyo wamchague kwa kura zote ili aweze kuwatua ndoo kina mama na kuleta maendeleo mbalimbali katika kata hiyo.

Katambi amewaomba wananchi hao kumchagua John Pombe Magufuli, Mbunge Patrobas Katambi na diwani wa Kata hiyo Paul Machela ambaye atawakilisha kero mbalimbali zilizopo na kuweza kutatuliwa.

"Najua kuna changamoto nyingi katika kata hii zikiwemo za kilimo, nichagueni mimi na Rais Magufuli ili tuweze kuwaletea matracta ya kulimia ambayo tutayaleta kwenye kata na mengine ya kuwakopesha"amesema Katambi.

Ameongeza kuwa katika sekta ya uchumi na biashara wataangalia ni namna gani kina mama waweze kujikwamua kiuchumi wakiwemo vijana wote,hivyo wataleta wataalamu ambao watawafundisha kina mama kutengeneza batiki na vitu vingine vya kimaendeleo.

Pia amewaomba wazee wamuamini waunde baraza la wazee ambalo litakuwa na viongozi litawasilisha kero zote zilizopo katika kata na zitafanyiwa kazi kwa wakati zikishindikana zitapelekwa bungeni na wazee watapata haki zao.

Kwa upande wake mgombea udiwani wa kata hiyo Paul Machela amesema  kuna kero ya daraja la kwenda Old Shinyanga daraja litaanza kujengwa na zahanati ya kijiji cha Bushola imekamilika, zahanati ya Mwamalili nayo imekamilika wanajenga maabara ikiisha tu tayari itaanza kutumika.

"Mimi ndiye diwani niliyekuwepo nawaambia ukweli, na Sasa nagombea ili tumalizie yaliyobaki, hivyo kila kitu kitakamilika ndani ya uongozi wa chama Cha mapinduzi na kwa kufuata ilani ya chama Cha mapinduzi CCM"amesema Machela.

Naye kampeni Meneja wa diwani Fulushi Matinde amesema nitamnadi Rais wangu Magufuli kwa sababu nazijua kazi zake pia nitamnadi Katambi kwa vile ni kijana anayejitambu 

"Niseme ukweli wa Machela alianza udiwani Mwaka 1995 enzi za mk upapa mpaka Sasa anaendelea kusimamia miradi mbalimbali zikiwemo zahanati,maji ya ziwa Victoria na maendeleo mengi mbalimbali"amesema Matinde.
 Christna Mzava mbunge viti maalumu kupitia Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga akiwa kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Mwamalili manispaa ya Shinyanga akiomba kura za diwani, mbunge na Rais wa chama Cha Mapinduzi CCM.Picha na Suzy Luhende.
 Mgombea Ubunge jimbo la Shinyanga Mjini akiendelea kunadi sera zake kuelekea October 28 
Mgombea udiwani kata ya Mwamalili manispaa ya Shinyanga akiomba kura kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata hiyo na kuhudhuliwa na mgombea ubunge Jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi.picha na Suzy Luhende
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464