KATAMBI AAHIDI SH MIL 30 ZAHANATI YA BUTENGWA, MATUNDU 8 YA VYOO, VYUMBA 5 VYA MADARASA NDEBMEZI



Na Shinyanga Press Club Blog

MBIO za kunadi sera na kuomba kura kwa wananchi katika Jimbo la Shinyanga Mjini mkoani Shinyanga zimezidi kupamba moto zikiwa zimebaki takribani siku 32 kabla ya zoezi la upigaji kura Oktoba 28, 2020.

Katika mbio hizo, Jana Septemba 26, 2020, Mgombe Ubunge wa jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi aliendelea na mikutano yake ya kampeni ili kuwafikia wananchi na kuwaomba kura, ambapo jana alikuwa katika Uwanja wa Mtaa wa Mabambasi Kata ya Ndembezi ambayo inaongozwa na diwani wa chama hicho, David Nkulila.

Akinadi sera na kutoa ahadi mbalimbali kwa wananchi wa kata hiyo, Katambi alisema wataibadilisha na kuwa na hadhi ya Mbezi ya Jijini Dar es Salaam, ambapo licha ya kupiga hatua mbalimbali za maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano ikiwemo ujenzi wa machinjio ya kisasa, barabara za lami na taa za barabarani, ameahidi mambo mbalimbali yatakayoipaisha kata hiyo.

Miongoni mwa ahadi hizo ni uboreshaji wa shule za Msingi Bugoyi A na B na sekondari ya Mazinge pamoja na zahanati ya Butengwa, ambapo amesema ifikapo mwaka 2021 atajenga vyumba vitatu vya madarasa na maabara vitakavyogharimu Sh Milioni 30 katika sekondari ya Mazinge, vyumba viwili vya madarasa na matundu sita ya vyoo katika Shule ya msingi Bugoyi vitakavyogharimu Sh Milioni 30.

Ahadi Nyingine ni matundu mawili ya choo shule ya sekondari Mazinge yatakayogharimu Sh Milioni 6, na kuiongezea Zahanati ya Butengwa Sh Milioni 30 kupitia fedha za mfuko wa jimbo ili iwe ya kisasa.

Tuna mipango ya kuleta maendeleo, kwa kushirikiana na Tarura tayari tuna barabara za mitaa ambazo zitatengenezwa kwa kiwango cha lami Km 4.2 lengo ni kuona mji wetu unakuwa na barabara nyingi za lami katika mitaa yetu,” alisema.

Kwa upande wake, Mgombea udiwani wa Kata ya Ndembezi ambaye pia anatetea nafasi hiyo, David Nkulila, aliwasihi wananchi kuichagua tena CCM kuhakikisha ilani inatekelezwa kama ilivyoahidiwa kwani huo ni mkataba baina ya wagombea hao na wananchi.

Nkulila alieleza kuwa ifikapo mwaka 2025 barabara zote zitakuwa na uwezo wa kupitika kwa wakati wote na pia wametenga eneo la ujenzi wa kituo cha polisi Butengwa kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama katika kata hiyo yenye  eneo la Km 20.5 za mraba na watu 22,288.

Nimekuwa mtumishi wa wanyonge, tumefanya kazi kubwa kumaliza migogoro ya ardhi na kituo cha afya kinajengwa….halmashauri yetu imedumaa kiuchumi hakuna mzunguko mkubwa wa fedha, hivyo nitahakikisha watendaji wa serikali hawawafungii wananchi biashara zao kwasababu ya leseni,” alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Abubakar Gulam amewaomba wananchi wa Ndembezi kumchagua David Nkulila kuwa diwani wa kata hiyo akidai kuwa Nkulila ni mtu mwenye msimamo na amekuwa mtetezi wa wanyonge na kupigania maslahi ya wananchi huku akiwaomba wamchague Katambi kuwa Mbunge kutokana na kwamba ni mtu wa kazi asiyependa porojo.

Nao baadhi ya wakazi wa kata ya Ndembezi waliohudhuria mkutano wa kampeni wamewataka wagombea hao  wa chama chama cha mapinduzi iwapo watashinda  katika uchaguzi mkuu octoba 28 wahakikishe wanatekeleza kwa vitendo yale ambayo yamehaidi katika kuyatekeleza  kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Mgombea Ubunge  jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi akinadi sera zake katika kata ya Ndembezi 

 Wagombea wa Udiwani Viti maalum Jimbo la Shinyanga Mjini wakiomba kura za Rais, Wabunge na madiwani ifikapo mwezi octoba mkutano uliofanyika katika viwanja vya Mabambasi kata ya Ndembezi  Kunadi sera za CCM kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga jana Septemba 25.
  Wagombea wa Udiwani Viti maalum Jimbo la Shinyanga Mjini wakiomba kura za Rais, Wabunge na madiwani ifikapo mwezi octoba mkutano uliofanyika katika viwanja vya Mabambasi kata ya Ndembezi  Kunadi sera za CCM kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga jana Septemba 25.

  Mgombea wa Udiwani Viti maalum Tarafa ya Ibadakuli Jimbo la Shinyanga Mjini akiomba kura za Rais, Wabunge na madiwani ifikapo mwezi octoba mkutano katika mkutano  uliofanyika katika viwanja vya Mabambasi kata ya Ndembezi  Kunadi sera za CCM kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga jana Septemba 25.
   Wagombea wa Udiwani Viti maalum Jimbo la Shinyanga Mjini wakiomba kura za Rais, Wabunge na madiwani wakiwa wamepiga magoti mapema jana kwenye mkutano katika kata ya Ndembezi 
 Mgombea Udiwani kata ya Ndembezi David Nkulila kulia akiwa ameshikiria ilani ya Chama Cha Mapinduzi itakayotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano yaani 2020-2025 
 Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abubakar Gulam akisikiliza namna ambavyo mgombea udiwani wa kata ya Ndembezi akiomba kura kwa wananchi 
 Wakazi wa kata ya Ndembezi wakiendelea kusikiliza sera za wagombea Udiwa ni na Ubunge CCM jimbo la Shinyanga Mjini 
  Wakazi wa kata ya Ndembezi wakiendelea kusikiliza sera za wagombea Udiwa ni na Ubunge CCM jimbo la Shinyanga Mjini 
  Wakazi wa kata ya Ndembezi wakiendelea kusikiliza sera za wagombea Udiwa ni na Ubunge CCM jimbo la Shinyanga Mjini 
 Mgombea Ubunge jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi akiendelea kuomba kura kwa wakazi wa ndembezi 
   Wakazi wa kata ya Ndembezi wakiendelea kusikiliza sera za wagombea Udiwa ni na Ubunge CCM jimbo la Shinyanga Mjini 
 baaadhi ya Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi jimbo la Shinyanga Mjini wakiendelea kusikiliza hoja za wagombea 
 Mgombea Ubunge Shinyanga Mjini Patrobas Katambi na Mgombea Udiwani Kata ya Ndembezi wakijiandaa kunadi sera zao.
 baaadhi ya Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi jimbo la Shinyanga Mjini wakiendelea kusikiliza hoja za wagombea
 Shughuli za kampenio zikiendelea Ndembezi 
Ishara ya umoja  kwa  wagombea wa udiwani na ubunge wakiwa wameshikana mikono  

Tazama picha  katika  matukio tofauti  picha zote na  Shinyanga  Blog 

  







  

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464