MAAFISA ELIMU KATA,WALIMU WAKUU NA VITENGO WAPATIWA MAFUNZO YA KUJENGEWA UWEZO WA USIMAMIZI ELIMU MAALUM


Na chausiku said 
Mwanza.

Shirika la Mwanza orphans ministry ( Mwaomi) jijini Mwanza limetoa mafunzo kwa maafisa elimu kata walimu wakuu shule za msingi na, sekondari na walimu wa vitengo maalum.

Mafunzo hayo ya Siku moja  yaliyofanyika katika shule ya msingi buhongwa wilaya ya Nyamagana yaliyolenga kuwapa walimu ujuzi na kuwajengea uwezo namana ya kuwasaidia watoto kwenye ulemavu na kutatua changamoto zao.

Mratibu wa shirika hilo Fredrick Eriakim ameeleza kuwa lengo kubwa la kutoa mafunzo hayo ni kutokana na changamoto mbalimbali zinanazowakabili watoto wenye mahitaji maalum.

Fredrick amesema kuwa kutoka na changamoto za miundombinu vifaa vya kufundishia pamoja na walimu kukosa takwimu sahihi ya watoto wenye mahitaji maalum katika jamii inayowazunguka ni muda mwafaka walimu kupata elimu hiyo ili kuweza kuwasaidia watoto hao.

"Sisi kama shirika ambalo liko chini ya kanisa tumajalibu kuzijadili changamoto na kuweka mikakati ya pamoja ambayo itatusaidia kupunguza changamoto hizo." Alisema Fredrick.

Fredrick alisema kuwa kutoka na mpango kazi walioutengeneza kwa kushirikiana na walimu kuhakikisha wanatekeleza pamoja kuleta matunda kwa watoto wenye mahitaji maalum.

Ameeleza kuwa moja ya mpango kazi  huo ni kuelimisha jamii kupita vyombo vya habari juu ya changamoto zinazowakabili watoto hao na wadau kijitokeza kuwasaidia kutatua changamoto hizo.

Afisa Elimu wa Elimu maalum Halmashuri ya Jiji la Mwanza Peter Ndomondo amesema kuwa mafunzo yaliyotolewa na shirika la Mwaomi yataleta manufaa makubwa kutoka na walimu wamepata uelewa na namana ya kusimamia shule zenye watoto wenye mahitaji maalum.

Peter ameeleza kuwa kutoka na wazazi wengi walikuwa wakiogopa kuleta watoto wenye ulemavu shuleni lakini kwa sasa Kadili walimu wanavyopata mafunzo wataweza kutatua changamoto zinazowakabili na kuelimisha jamii inayowazunguka kuwaleta watoto ili waweze kupata elimu kama watoto wengine.

"Miaka ya nyuma kulikuwa na changamoto kadhaa juu ya uelewa mdogo kwa watu wenye mahitaji maalum na kuwaona wao ni mizigo kwa sasa wamepata elimu inayowasaidia kuwaona watu wenye mahitaji maalum wanauwezo kama wengine.

Zakia Mohammed Mwalimu Mkuu wa vitengo cha wanafunzi mwenye ulemavu wa akili, usonji na viziwi ameeleza mafunzo yatawasaidia kutoka elimu kwa walimu wakuu na wanafunzi wa sio na ulemavu ili na wao wawe mstari wa mbele kuhakiksha wanatoa elimu juu ya watoto wenye ulemavu ili kuleta usawa kwa watoto wote.


Kambalame Abdallah kutoka ni Mwalimu kutoka shule ya Msingi Nyamalango ambaye sio mwalimu wa Elimu maalum amesema kuwa mafunzo hayo waliyoyapata yatawasaidia kwa kiwango kikubwa hata mwalimu husika wasipo kuwepo na watakapohitaji msaada watawasaidia.

" nimejifunza mambo mengi jinsi ya kuwasaidia, lakini pia nimefahamu baadhi ya alama mbalimbli zitakazonifanya kuweza hata kuzungumza nao" alisema kambalame.

Kambalame amesema kuea changamoto mbalimbali zinazowakabili walimu na wanafunzi wenye mahitaji maalum ikiwa  ni pamoja na mazingira kutokuwa rafiki hivyo kusababisha watoto wenye mahitaji maalum kushindwa kufikia malengo yao.

Aidha wametoa wito kwa serikali na taasisi mbalimbali kuweza kushirikiana kuweza kutatua changamoto zinazowakabili watoto wenye mahitaji maalum kwani na wao wanahitaji kusoma katika mazingira rafiki kama watoto wasiokuwa na ulemavu.





Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464