MAJALIWA ATANGAZA VITA WANAOWATOZA FEDHA WAJAWAZITO NA WAZEE


Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

WATENDAJI waliopo kwenye Vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali za Wilaya, wanaowatoza fedha Wajawazito, watoto walio chini ya miaka mitano na wazee wanapohitaji huduma za afya kukiona cha mtemakuni kwani wanaofanya hivyo wanakwenda kinyume na sera ya afya nchini.

Hayo yalibainishwa jana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kisamba Kata ya Lubugu na Ilungu Kata ya Nyigogo wilayani Magu akiwa njiani kuelekea jijini Mwanza akitokea mkoani Mara.

Alisema sera hiyo inatekelezwa kwenye hospitali zote hivyo anapotokea mtu anaiharibu washughulike naye kwa kuwa Serikali iliyopo ni ya kuwashugulikia watu wasio na uelevu hivyo wananchi watoe taarifa pindi wanapopatwe na adha hiyo.

"Tiba ya mama mjamzito ni bure ata kujifungua, watoto na wazee tumeleta fedha billion 10.8 kwa nini watozwe hela wakati fedha zipo kama kuna mtendaji anayewatoza hao niliowataja wachukuliwe hatua kwa sababu ni wauwaji pia tumewaboreshea vituo vya afya vyote ni vya kisasa kuna sehemu ya kupima magonjwa yote chumba cha upasuaji mdogo,wakati na mkubwa sambamba na chumba cha mama na mtoto "alieleza Majaliwa.

Alisema Magu bado kuna changamoto ya vituo vya afya, Serikali itajenga vingine ingawa imekamilisha vituo vya afya Kahangara (Sh. bilioni 1.4), Lugeye (Sh. milioni 400) na Kabila (Sh.milioni 400) ambapo kituo cha Kahangara kitaongezewa Sh. milioni 400, pia itatoa Sh. milioni 200 za upanuzi wa Hospitali ya Wilaya ya Magu.
 
Pia vimejengwa vituo vya afya vya kimkakati na vyote vina huduma zote ambapo kutokana na mahitaji ya dawa kuongezeka wametoa Sh. bilioni 10.8 ili kuwezesha upatikanaji wa dawa ili wananchi wasiendelee kununua kwenye maduka binafsi.

Alisema Serikali iko kwenye mchakato wa kutekeleza muswada wa Bima ya Afya kwa Watanzania wote wapate matibabu na itatoa magari ya kubeba wagonjwa mahututi na wa dharura hasa wajawazito kwenye vituo vyote vya afya nchini vikiwemo vya Wilaya ya Magu. 
 
"Endapo wananchi wa Magu wataichagua CCM mkakati wa Serikali ni kuhakikisha wilaya hiyo inapata maji ya uhakika na tayari imepeleka Shilingi bilioni 23 .3 za miradi ya majina kufafanua kuwa mradi wa maji kwenye vijiji vya Kinango (Sh.milioni 107),Matela (sh.milioni 397), Kabale (sh.milioni 231),Buhumbi, Bugatu, Ndagalu, Nyasato (sh. bilioni 2.1) na Nsolo (sh.Bilioni 1)," alisema.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464