Nahodha wa Tanzania
Mbwana Samatta amejiunga na Club ya Fenerbahce ya Uturuki akitokea Aston
Villa ya England, bado Fenerbahce haijaweka wazi kama wamemsajili kwa
mkopo wa msimu mzima 2020/21 kama inavyoripotiwa au ni uhamisho kamili
Fenerbahce wamempa jezi namba 12 Mbwana Samatta ambaye anaenda kuongeza
nguvu katika kikosi hicho, club hiyo imewahi kumuwania mara kadhaa hata
kabla ya kwenda Aston Villa lakini ndoto ya Samatta ilikuwa ni kucheza
EPL.
Hata hivyo vyanzo vingine vya habari akiwemo Mwandishi nguli Salim Kikeke vimeeleza kuwa Fernabache wametangaza kumsajili Samatta kwa mkataba wa miaka minne, huku Wawakilishi wa Mbwana Samatta wakieleza kuwa usajili huo ni usajili mkubwa kufanyika katika dirisha hili la usajili nchini Uturuki.
Mbwana Samatta akiwa na wawakilishi wake pamoja na viongozi wa klabu ya Fenerbahçe S.Kni baada ya kukamilisha usajili wake
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464