LEO Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo, Bernard Membe amezindua kampeni zake mkoani Lindi, akiambatana na baadhi ya viongozi wa chama hicho akiwemo Zitto Kabwe na hizi ni sehemu ya kauli walizozitoa.
"Ndugu zangu wa Lindi tukitaka kwenda Ikulu tufanye haya, kwanza tuondoe uoga Oktoba 28 akili kichwani, unaondoka zako unaenda kwenye kile chumba unamuangalia mtoto wa nyumbani anatabasamu na lile tabasamu siyo la bure ni la kuwaambia watanzania hapa ndiyo penyewe" - Bernard Membe
"Sisi watu wa Pwani na sisi ACT WAZALENDO na mimi nikiwa Rais wenu hatutawabugudhi wavuvi, Dagaa ni Dagaa ataliwa tu, iwe awe na wavu mdogo mtavua kwa taratibu zitakazoruhusu hakuna Mvuvi atakayechomewa Nyavu zake" - Bernard Membe
"Miaka 5 sasa imetimia tangu CCM kipewe ridhaa ya kuwaongoza Watanzania, 2015 vyama vyote tulikuja kwenu Watanzania na Ilani zetu mtuunge mkono, wenzetu wa CCM wakapewa kazi, miaka 5 CCM wamekuwa wakikusanya kodi na kuzitumia kwa niaba yetu," amesema Zitto.
"Tumekuja kuzindua kampeni Lindi kwa sababu tumeamua tuanze na mguu mzuri kwani mgombea wa Urais Mh Bernard Membe anatokea huku na amewakilisha vizuri kwa vipindi vitatu 2000-2015 akiwa Mbunge wa Mtama, naamini kuanzia kesho safari yetu itakuwa njema," amesema Zitto.
"Tumekuja kuzindua kampeni Lindi kwa sababu tumeamua tuanze na mguu mzuri kwani mgombea wa Urais Mh Bernard Membe anatokea huku na amewakilisha vizuri kwa vipindi vitatu 2000-2015 akiwa Mbunge wa Mtama, naamini kuanzia kesho safari yetu itakuwa njema," amesema Zitto.
Sehemu ya wafuasi na wanachama wa ACT Wazalendo waliohudhuria uzinduzi wa kampeni za Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama hicho, Bernard Membe leo mkoani Lindi
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464