Na Marco Maduhu
Shinyanga.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Shinyanga mjini kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Salome Makamba ameonyesha kusikitishwa na mkoa wa Shinyanga kudumaa kimaendeleo, licha ya kuwa na utajiri mkubwa wa rasimali za madini ya Dhahabu na Almasi.
Makamba amebainisha hayo jana kwenye uzinduzi wa kampeni za chama hicho jimbo la Shinyanga mjini, uliofanyika katika eneo la Ngokolo, na kuhudhuliwa pia na wagombea udiwani wa Kata zote 17 za Manispaa ya Shinyanga, pamoja na viongozi wa chama hicho.
Amesema endapo wananchi wakimpigia kura siku ya uchaguzi Oktoba 28 mwaka huu na kushinda kuwa mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini, atakwenda bungeni kupigania ukuaji wa maendeleo ya mkoa wa Shinyanga, ili uendane na utajiri uliopo wa madini ya Dhahabu na Almasi.
“Mkoa wa Shinyanga una utajiri mkubwa sana wa madini ya dhahabu na almasi, lakini ukiangalia hauendani kabisa kimaendeleo na utajiri uliopo, na mkoa huu ni wa tano kuchangia pato la taifa, hivyo naombeni mnipe ubunge ili nikapambanie maendeleo ya mkoa wetu,” amesema Makamba.
“Mbali na kupigania maendeleo ya mkoa wetu huu, pia ni tahakikisha mnanufaika na rasilimali zilizopo za madini kuinuka kiuchumi, na siyo kupewa mchanga wa marudio wa madini ya Almasi na mgodi wa Almasi Mwadui, ambao hauna kitu,” ameongeza.
Pia Mgombea ubunge huyo amewahakikishia wanawake na vijana watapata fedha za kufungua biashara mbalimbali kupitia fedha za mfuko wa jimbo, kwa kuunda vikundi vya ujasiriamali, ambazo ndani ya miaka 10 iliyopita hawakunufaika nazo.
Katika hatua nyingine Makamba amesema akienda bungeni atapambana kutokomeza tatizo la mimba na ndoa za utotoni, ambalo limekuwa changamoto kubwa ya kuzima ndoto za wanafunzi wa kike, pamoja na kupeleka ajenda ya kupigania wanafunzi wanaopewa ujauzito waruhusiwe kuendelea na masomo yao ili watimize malengo yao.
Amesema kuna wanafunzi wengine wanapewa ujauzito bila ya kutarajia huenda kwa kubakwa, hivyo ukimfukuza shuleni ni kumnyima haki yake ya kielimu sababu haikuwa dhamira yake kuzima ndoto zake.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mgombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini kupita chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Salome Makamba akinadi sera kwa wananchi wa Shinyanga ili wampigie kura na kuwa mbunge wa jimbo hilo kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 28 mwaka huu.
Meneja Kampeni wa mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Salome Makamba, Juma Ptotas akiwataka wananchi wa Shinyanga wasifanye makosa Oktoba 28 bali wampigie kura Makamba.
Wagombea udiwani, na mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Salome Makamba akiwa na baadhi ya viongozi wa chadema kwenye uzinduzi wa kampeni.
Wananchi wakisikilza sera za mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Salome Makamba wa Chadema.
Wananchi wakiwe eneo la mkutano wakiendelea kusikiliza sera za mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Salome Makamba.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.