Mgombea Ubunge jimbo la Solwa kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ahmed Salum akiwaomba wananchi wamchague tena kuwa Mbunge wa Jimbo la Solwa.
Na Shinyanga
Press Club Blog
Mgombea
Ubunge jimbo la Solwa kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ahmed Salum anayetetea
kiti chake amewaomba wapiga kura wa jimbo hilo wamchague tena kwa kumuongezea miaka mitano tena ili aendelee kuwaletea
maendeleo katika Nyanja mbalimbali ikiwemo sekta ya maji,uchimbaji mdogo na
afya.
Akizungumza wakati
wa uzinduzi wa kampeni katika jimbo hilo zilizofanyika kata ya mwakitolyo Ahmed
amesema kuwa anazitambua changamoto na kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Solwa ikiwemo
miundombinu ya barabara huku akidai kuwa baadhi ya barabara hizo zipo katika
utekelezaji wa uboreshaji.
"Kama mnavyofahamu jimbo letu tunazidi kupambana kutatua kero zinazolikabili ambapo mnafahamu barabara yetu ya Kahama Mwakitolyo hadi Mwanza imekuwa ikikatika mara kwa mara na kukosesha mawasilaiano lakini kwa sasa hali ni tofauti tayari ufumbuzi wa kudumu umeanza kupatikna ikiwemo kujengwa kwa makaravati makubwa"
Ahmed ameendelea kuwaomba wapga
kura wa jimbo hilo wamchague kuwa Mbunge
wao pamoja na Rais Magufuli na madiwani wa CCM kwani Ilani ya uchaguzi ya CCM ya
mwaka 2020-2025 inagusa maisha ya Watanzania na CCM imedhamiria kuwaletea
maendeleo wananchi huku akigusia suala la wachibaji wadogo
"Kwenu ninyi wakazi wa mwakitolyo mlikuwa mkisumbuliwa sana na utozaji wa kodi ya shilingi laki moja lakini mmesikia maagizo ya Mheshimiwa rais nami nimeshaanza kutekeleza na sasa hiyo kodi haipo wala hakuna usumbufu tena fanyeni kazi zenu kwa amani na usalama zaidi "
Akimnadi Mgombea ubunge wa jimbo
hilo Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa amewaomba wananchi
kuchagua wagombea wa CCM ili waweze kuwaletea maendeleo yatakayowanufaisha
wananchi.
Naibu Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mgombea
Ubunge aliyepita bila kupigwa katika jimbo la Ushetu wilayani Kahama Elias
Kwandikwa amesema Serikali ya CCM inaendelea kuboresha miundombinu ya barabara
pamoja na utoaji wa maeneo kwa wachimbaji wadogo wadogo katika eneo la
Mwakitolyo hivyo ni muhimu kwa wachimbaji kuchangamkia fursa hiyo.
"Hali ya eneo la Mwakitolyo pale wakati wa msimu wa mvua palikuwa pakikatika mara kwa mara na kuwapa usumbufu wananchi wanapotakiwa kwenda kupata mahitaji hadi wazunguke kahama na kwenda shinyanga ambapo ni mbali sana sasa ufumbuzi umepatikana kwani serikali imetoa fedha na zoezi la ukwekaji Makaravati makubwa unaendelea"
Kwandikwa ameongeza kuwa serikali ilikuwa ikitoa hilingi milioni 900 kufanya marekebisho ya dharura katika eneo hilo wakati mvua zinapokuwa nyingi na kupelekea kusombwa kwa eneo hilo na wananchi walilazimika kutumia mitumbwi kuvuka kutoka eneo moja hadi jingine
Kwa upande wake Mjumbe wa NEC,
Gaspar Kileo ambaye pia ni Meneja kampeni wa mgombea ubunge jimbo la Shinyanga
mjini. Patrobas Katambi amewataka wapiga
kura kuchagua wagombea wa Chama Cha Mapinduzi ili waendelee kutekeleza ilani
yao katika kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo la Solwa.
wakimuombea kura mgombea ubunge
jimbo la Solwa,Wagombea Ubunge wa viti maalumu Mkoa wa Shinyanga Lucy Mayenga
na Santiel Kirumba wamewaomba wanawake
kumpigia kura Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Tanzania ,Wabunge pamoja na
madiwani wa CCM hali itakayosaidia
kuleta maendeleo kwa ushirikiano.
Katika hatua
nyingine wagombea hao wamewataka wachimbaji wadogo kuendelea kuchimba madini ya
dhahabu kwa kujiamini bila kubughuziwa wakati serikali ikiendlea kutatua changamoto
zao
Mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Solwa akiendelea kunadi sera zake kwa wapiga kura wa jimbo hilo
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Solwa akiwasili katika uwanja wa Mwakitolyo kwa ajili ya kunadi sera zake
Wananchi na wanachama wa CCM wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi
Wananchi na wanachama wa CCM wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi
Baadhi ya Wagombea wa nafasi ya udiwani kutoka jimbo la Solwa wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa mbele ya wananchi wa Mwakitolyo
Mgombea ubunge viti Maalum mkoa wa Shinyanga Dr Christna Mzava akipiga Magoti akimuombea kura Rais,Mbunge na Madiwani wa jimbo la Solwa
Kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi ambaye ni Mgombea Ubunge aliyepita bila kupigwa katika jimbo la Ushetu Elias Kwandikwa akiwaombea kura wagombea wa CCM. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa
Mgombea Ubunge jimbo la Solwa kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ahmed Salum akiwa kwenye mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za CCM ambapo amewaomba wananchi wamchague tena kuwa Mbunge wa Jimbo la Solwa.