Wa pili toka Kushoto ni Mgombea Nafasi ya Urais kupitia Chama Cha (ADA TADEA) Mh. John Shibuda akimkabidhi baadhi ya Nyaraka mgombea ubunge jimbo la Maswa Magharibi Bi Lydia Mbuke Bendera ili atakapopata ridhaa ya wapiga kura akatekeleze kwa vitendo.
Mgombea Ubunge jimbo la Maswa Magharibi kupitia chama cha
ADA TADEA Bi Lydia Mbuke Bendera amesema
kuwa iwapo atapata ridhaa ya kuwawakilisha wakazi wa jimbo hilo atahakikisha anatimiza vipaumbele vyake kumi ikiwemo upatikanaji wa fulsa mbalimbali za ajira kwa vijana pamoja na tatizo la maji.
Akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni Jimbo la Maswa Magharibi katika kata ya Malampaka Mgombea huyo amesema
kuwa kumekuwapo na changamoto kubwa ya tatizo la ajira nchini hususani kwa
kundi kubwa la vijana.
“Suala
la Ajira litakuwa ndoto kwa wana Maswa Magharibi kama mkinipatia mimi nafasi ya
kuwawakilisha na kuwapigania bungeni
kwani mimi niko makini kwenye utafutaji wa fulsa za uwekezaji zitakazosaidia
kupunguza tatizo la ajira me nawahakikishia tutakwenda wote bega kwa bega hususani kwa vijana wa darasa la saba,kidato
cha nne na vyuo vya kati wataweza kuendesha maisha yao”
Lydia ameongeza kuwa iwapo ataingia bungeni atapambana
kadri ya uwezo wake kubuni fulsa za biashara kwa wakazi wa malampaka na jimbo
zima la Maswa Magharibi ili wananchi waweze kufanya biashara kulingana na
maeneo yao huku akiahidi kuboresha sekta binafsi kwa kushirikiana na wakazi wa
jimbo hilo,kuunganisha jimbo lote kwa miundombinu ya barabara, kuweka mfumo
rafiki wa kupokea changamoto za wananchi wake pamoja na kusimamia ujenzi wa
hospiatal kutokana na uchache wa vituo vya afya.
“Kwa
hiyo ndugu zangu wana Malampaka na Jimbo zima la Maswa Magharibi nina amini
haya yote yanawezekana mkinipa fulsa ya kwenda jijini Dodoma kuwakilisha hizi
hoja itakuwa rahisi na vyepesi kwa sababu shida zenu nyingi nazifahamu hivyo
kuweni na imani na mimi ndugu zangu hakikisheni tarehe 28 mwezi wa kumi
hamfanyi makosa”
Kwa upande wake Mgombea udiwani kata ya Malampaka kupitia
ADA TADEA Charles Mwinuka amewaomba wakazi wa kata hiyo kumpatia kura
zitakazosaidia yeye kwenda kuwawakilisha kwenye baraza la madiwani ambapo
amehaidi kuanza na kero kubwa na muda mrefu ya kero maji, barabara na umeme
“Ukiangalia
kwa sasa watoto wadogo unawakuta kwenye Malambo ya maji akienda
kutafuta maji ili hali huu ni mji mkongwe wa muda mrefu sana ambao ulipaswa
kuwa na huduma za maji toka ziwa Victoria,angalia barabara zetu hazilingani na
mji huu kwa hiyo nipeni nafasi nikawatete kwenye halmashauri huko”
Naye Mgombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kupita ADA TADEA Mh John Shibuda amewataka wakazi wa jimbo la Maswa Magharibi
kuchagua viongoiz ambao ni sikio la
wananchi wanaosikiliza na kutatua kero zao ambao wanatoka katika chama chake
“Najua
Mnajua maana ya uongozi mbovu ninaomba muelewe
ninapowaambia kuwa ukiwa na mbunge ambaye siyo sikio la wanachi ni changamoto
tu, pale ambapo tuliwahitaji wao
hawakutuitaji,tusipowahitaji wao ndo wanatuhitaji hii ndiyo shida ya kuwa na
wabunge wasio kuwa sikio la wananchi”
Mheshimiwa Shibuda amemtaka Mgombea huyo wa nafasi ya
ubunge iwapo atapata ridhaa ya wananchi hakikisheni anakwenda kusimamia na
kukamilisha yale yote ambayo yeye wakati akiwa mbunge wa jimbo aliyaanzisha
ikiwemo ujenzi wa mabwawa ya maji yatayosaidia kukabiliana na majanga ya ukame
na uharibifu wa mazingira
Mheshimiwa Shibuda amebainisha kuwa jimbo la Maswa
Magharibi bado linakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya wafugaji, kilimo
cha zao la pamba,umeme kwa baadhi ya vijiji kutokuwa na nishati hiyo na
kuchangia wananchi kushindwa kwenda na wakati wa sasa wa sayansi na teknolojia
“Wakati
nikiwa Mbunge wa jimbo hili kabla ya kuwania Nafasi ya Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania niliacha jimbo hili la Maswa Magharibi likiwa asilimia 95 za huduma ya umeme yaani sehemu
kubwa ya vijiji vyake vina umeme lakini leo kuna vijiji havijapata umeme mpaka
leo ambayo ni sawa na asilimia 5 kwa
hiyo mgombea wangu nakukabidhi barua na maadishi ya wapi nilihishia ili nawe
uanzie hapo”
Mgombea Nafasi ya Urais kupitia Chama Cha (ADA TADEA) Mh. John Shibuda akiwa ameketi pamoja na Mgombea ubunge jimbo la Maswa Magharibi Bi Lydia Mbuke Bendera wakiendelea kutazama burudani zinazoendelea.
Mgombea Nafasi ya Urais kupitia Chama Cha (ADA TADEA) Mh. John Shibuda akiwa ameketi pamoja na viongozi mbalimbali wa chama pamoja na Mgombea ubunge jimbo la Maswa Magharibi Bi Lydia Mbuke Bendera wakiendelea kutazama burudani zinazoendelea.
Baadhi ya Machifu wa kabila la kisukuma wakiwa wameketi kwa pamoja wakiendelea kuteta jambo juu ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu
Baadhi ya wakazi wa kata ya Malampaka Jimbo la Maswa Magharibi wakiwa wamesimama wakiendelea kusikiliza hoja za wagombea toka (ADA TADEA)
Watoto nao hawakuwa mbali kusikiliza sera za wagombea waliofika kunadi katika eneo la Malampaka wakiwa na wazazi wao kwa pembeni ili kuhakikisha wanapatikana viongozi bora na makini
Mgombea ubunge jimbo la Maswa Magharibi Bi Lydia Mbuke Bendera akielekea jukwaani kunadi sera zake huku akisindikizwa na baadhi ya wanachama wa chama hicho katika mkutano uliofanyika Malampaka.
Wananchi wakiendelea kusikiliza sera za wagombea
Wa pili toka Kushoto ni Mgombea Nafasi ya Urais kupitia Chama Cha (ADA TADEA) Mh. John Shibuda
akimsisitizia jambo mgombea ubunge jimbo la Maswa Magharibi Bi Lydia Mbuke Bendera ili atakapopata ridhaa ya wapiga kura akatekeleze kwa vitendo awe mfano wa kuigwa na jamii ili atakapoondoka awe ameacha alama.
Mgombea Nafasi ya Urais kupitia Chama Cha (ADA TADEA) Mh. John Shibuda akiwakumbusha wapiga kura kuwa siku ya uamuzi sahihi ni octoba 28 mwaka huu
Baadhi ya Machifu wa Kabila la Wasukuma wakiwa katika mkutano wa wa wagomea Urais na Ubunge Kutoka ADA TADEA katika kata ya Malampaka jimbo la Maswa Magharibi
Baadhi ya Machifu wa Kabila la Wasukuma wakiwa katika mkutano wa wa wagomea Urais na Ubunge Kutoka ADA TADEA katika kata ya Malampaka jimbo la Maswa Magharibi
wananchi wakiendelea kusilikiza hoja wa wagombea
Mmoja wa Wagombea wa Ubunge Kupitia ADA TADEA akimnadi Mgombea ubunge jimbo la Maswa Magharibi