MGOMBEA UDIWANI AAHIDI KUIBUA VIPAJI

 

 Mwenyekiti wa mtaa wa Dome kata ya Ndembezi Solomon Nalinga Najulwa 'maarufu Cheupe Plastiki' akimnadi mgombea udiwani kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga, Victor Mkwizu (kushoto).
Mgombea udiwani kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga, Victor Mkwizu akinadi sera za CCM na kuomba achaguliwe kuwa diwani wa kata ya Ngokolo.
Mgombea udiwani kata ya Ngokolo, Victor Mkwizu akiwa katika ofisi ya CCM kata ya Ngokolo baada ya kumaliza mkutano wa hadhara na wananchi hao kumsindikiza kutoka mtaa wa Kalonga mpaka ofisi ya CCM kata
Khamisa Magulu ambaye alikuwa mtia nia wa ubunge Jimbo la Shinyanga akimuombea kura Victor Mkwizu.

Na Suzy Luhende, Shinyanga
Mgombea udiwani kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga Victor Mkwizu amewaomba wananchi wa kata ya Ngokolo wampe kura, ili aweze kufanya maendeleo na kuanzisha michezo kwa kuibua vipaji mbalimbali kwa vijana kwa kuwa michezo ni ajira.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika mtaa wa Kalonga kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga, Mkwizu alisema anaomba kura zote ili ashinde aweze  kuanzisha michezo na kuibua vipaji mbalimbali kwa wanamchezo wote wa kata hiyo.

"Chama Cha Mapinduzi kipo kwa ajili ya wananchi na kwa ajili ya vijana kufanya maendeleo na kutatua changamoto zote zilizopo katika kata hiyo, na pia tutaziwekea moramu Barabara zote zinazosumbua katika kata hii",alisema Mkwizu.

Kwa upande wake Khamisa Magulu ambaye alikuwa mgombea wa ubunge Jimbo la Shinyanga mjini akitokea kata ya Ngokolo aliwaombea Kura wagombea wote kuanzia Rais John Pombe Magufuli, Patrobas Katambi kuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini na Victor Mkwizu ambaye ndiye mgombea udiwani kata ya Ngokolo kupitia CCM.

"Niwaomba sana ndugu zangu mpeni  kura zote Rais Magufuli mgombea urais, Patrobas Katambi mgombea ubunge na mimi niwe diwani wenu, kwa kushirikiana na viongozi hao tuweze kuleta maendeleo zaidi kupitia usimamizi wa chama cha mapinduzi CCM,"alisema Magulu.

Naye Khamis Kado mwenyekiti wa wazazi kata ya Ngokolo aliwaomba wananchi wa kata ya Ngokolo wasikubali kupewa rushwa ya shilingi 20000, badala yake wamchague kiongozi mwadilifu anayetoka chama Cha Mapinduzi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464