MGOMBEA WA UMD KIGOMA KUSINI ATAKA WANANCHI WAMCHAGUE WA CCM


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini kwa tiketi ya chama cha UMD, Zainab Bashange (kushoto) akikabidhiwa fomu ya uchaguzi

MGOMBEA ubunge wa jimbo la Kigoma Kusini kwa tiketi Chama cha UMD, Zainabu Bashange amewataka wapiga kura katika jimbo hilo kutopoteza muda wao kufikiria nani wa kumchagua badala yake amewataka wapiga kura kumchagua mgombea wa CCM, Nashon Bidyanguze.

Alisema hayo akihutubia kampeni za uchaguzi mkuu katika jimbo hilo uliofanyika kijiji cha Nguruka Kati, wilaya ya Uvinza mkoani.

Bashange alisema kuwa pamoja na wapinzani kugombea kama takwa la demokrasia lakini anaamini mgombea wa CCM atawavusha wananchi kimaendeleo hivyo kura zao zielekezwe kwa mgombea huyo kwa maendeleo ya jimbo hilo.

Katika Mkutano huo ambao ulihudhuriwa pia na viongozi wengine wa vyama vya siasa akiwemo Katibu wa TADEA mkoa Kigoma, Mandela Daniel na  Mwenyekiti wa CCK mkoa, Selemanu Msanum, mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Nashon Bidyanguze alisema kuwa atatumia ilani ya uchaguzi ya CCM kutekeleza mipango yake ya maendeleo kwa ajili ya wananchi kwa kuweka vipaumbele ambavyo vimo kwenye Ilani hiyo. 

Kigoma alisema kuwa pamoja na hilo atasimama kuhakikisha Kijiji cha Nguruka Kati kinapandishwa hadhi na kuwa mji mdogo.

“Nina nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi wa jimbo hili, kuna rafiki zangu wanaishi Marekani waliniita nikaishi huko nikaenda nikakaa kwa muda baadaye nikaenda Canada lakini sikuweza kuishi muda mrefu huko maana dhamira yangu ni kuwatumikia Watanzania masikini ndiyo maana nimerudi nyumbani kuja kuungana nanyi tuweze kusimamia maendeleo yetu,” alisema Bidyanguze.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464