Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya (kushoto) akizungumza na watumishi wa tume hiyo wakati alipotembelea mabanda ya taasisi mbalimbali zilizopo chini ya wizara ya Madini kwenye maonesho ya tatu ya teknolojia na uwekezaji katika sekta ya madini yanayofanyika kwenye Uwanja wa Bombambili mjini Geita.
Na Mwandishi Wetu, Geita
Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya leo Septemba 27, 2020 ametembelea mabanda ya Wizara ya Madini kwenye maonesho ya teknolojia na uwekezaji kwenye sekta ya Madini yanayoendelea katika uwanja wa kituo cha uwekezaji Bombambili, mjini Geita.
Mara baada ya kutembelea banda la Tume ya Madini kwenye maonesho hayo, Prof. Manya amepongeza kazi nzuri iliyofanywa na wataalam wa tume hiyo na kuwataka kuendelea kuelimisha umma hasa wachimbaji wadogo kuhusu Sheria ya Madini na kanuni zake, usalama wa afya na mazingira wanapoendesha shughuli za uchimbaji na biashara ya madini.
Profesa Manya (kulia) akisaini katika kitabu cha wageni baada ya kutembelea banda la Tume ya Madini
Profesa Manya (kulia) akisikiliza maelezo katika banda la kituo cha Jemolojia
Prof. Manya akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Wizara ya Madini
Profesa Manya (katikati) akikagua moja ya machapisho kwenye banda la wizara ya madini
Mmoja wa maofisa wa Tume ya Madini (kulia) akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali kwa Katibu Mtendaji wa Tume hiyo, Profesa Shukrani Manya (kushoto)
Profesa Manya akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) mbele ya banda la tume hiyo kwenye uwanja wa Bombambili mjini Geita
Watumishi wa Tume ya Madini wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mtendaji wa tume hiyo, Profesa Shukrani Manya (katikati) mbele ya banda la tume hiyo kwenye maonesho ya teknolojia na uwekezaji katika sekta ya madini mkoani Geita.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464