TAKUKURU YAREJESHA SHAMBA LA EKARI 4.5 KWA WATOTO WALILOZUNGUSHWA MIAKA 16 NA BABA YAO MKUBWA



TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kilimanjaroimefanikiwa kurejesha shamba la urithi la ekari nne na robo kwa watoto wa marehemu Antony Samba baada ya kuzungushwa kwa takribani miaka 16 bila mafanikio na baba yao mkubwa ambaye alikuwa ni msimamizi wa mirathi.

Shamba hilo lipo eneo la Mabungo, Uchira nje kidogo ya mji wa Moshi ambalo lilikuwa likabidhiwe kwa watoto wa marehemu Antony Samba aliyefariki mwaka 2004.



Katika hatua nyingine, TAKUKURU mkoa wa Arusha imemkabidhi mwananchi, George Chacha mkazi wa mtaa wa Olasiti namfanyakazi wa kampuni ya Heritage Energies ya jijini Arusha kiasi cha Sh Milioni 2,530,000 alizokuwa anaidai kampuni ya Temi Investiments Ltd ya jijini humo tangu mwezi Desemba, mwaka jana.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464