Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Tanesco(Katikati aliyevaa Miwani)akiwa pamoja na wajumbe wa bodi hiyo pamoja na watendaji wa tanesco Mkoa wa Shinyanga na baadhi wa watumishi wa Tanesco wakiangalia namna utekelezaji unavyoendelea juu ya ukamilishaji wa Kituo hicho eneo la Bulyanhulu Kahama.
Na Kareny Masasi Shinyanga Press Blog
Na Kareny Masasi Shinyanga Press Blog
Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme nchini
(Tanesco) Dr. Alexander Kiyaruzi amesema kuwa ameridhishwa
na hali ya ujenzi wa kituo kidogo (substation) kitakachohusika kulisha Mkoa wa Geita uzalishaji wa
Umeme kilichopo Bulyanhulu wilayani Kahama Mkoani Shinyanga kitachaongeza nguvu ya kusambaza umeme katika Mkoa wa Geita na kupelkea uwepo wa umeme wa uhakika.
Dakta Kiyaruzi amesema hayo jana alipotembelea kituo hicho kilichopo Bulyanhuru na kusema kuwa uwepo wake utasaidia kuondoa kero ya umeme kutotosheleza mahitaji ya wateja katika Mkoa wa Geita na baadhi ya Maeneo ya wilaya za mkoa wa Kagera na kuwa kukamilika kwake kutaifanya Geita kuwa na umeme mwingi na wa uhakika .
“ Umeme utakuwa na nguvu kubwa ya uhakika unaotoka katika kituo kidogo cha Bulyanhulu nategemea kitaaanza kazi hivi karibuni ndani ya mwezi huu wa tisa ambapo lengo la serikali ni kuhakikisha uwepo wa umeme wa uhakika nchini ikiwezana tuuze nje kwani mahitaji ya Mgodi wa Geita ni Kilovati 30 hivyo itasaidia sana" amesema Dakta Kiyaruzi
amesema kituo hicho kitaongeza nguvu ya nishati hiyo kwa mikoa hiyo kwani kitakuwa na kilovati 220 na kupunguza hasara waliyokuwa wakiipata kwa kusafirisha umeme mdogo kutoka eneo la Ibadakuli lililopo Mjini Shinyanga ambapo ameridhika na maendeleo yake na kuwa ifikapo Septemba 14 umeme utawashwa kwa ajili ya kuanza kutoa huduma .
Dakta Kiyaruzi amesema kutokana na kuwepo kwa viwanda na shughuli za madini umeme uliokuwepo ulikuwa hautoshelezi mahitaji na kuamua kuongeza nguvu kwa kujenga kituo hicho kipya
“Kutakuwepo na laini nyingine maeneo ya Nyakanazi itayopelekea Umeme mkoani Kigoma pia Mpanda mkoani Katavi kwenda Iringa ,Tunduma hadi Sumbawanga na mkoa wa Songwe maeneo hayo umeme utakuwepo wa uhakika lengo ni uhakika wa umeme nchi nzima hivyo watanzania wajiandae tu kwa kukuza uchumi wao kupitia sekta ya umeme ”amesema Kiyaruzi.
Kwa upande wake mjumbe wa bodi ya wakurugenzi Tanesco Dakta John Kihamba amesema kuwa Serikali inaboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo umeme ili kukuza uchumi wa nchi katika mazingira Mazuri ikiwemo umeme wa uhakika utakaosaidia kuvutia uwekezaji wa aina mbalimbali ikiwemo viwanda,madini na vinginenvyo
"Mipango ya Tanesco ni kuhakikisha kwamba kila mwananchi anapata umeme tena umeme wa uhakika kwa hatua amabzo zimefikia hapa umeme kwa mkoa wa Geita kwa sasa upo wa kutosha kwa hiyo yule anayehitaji kuanzisha shughuli zinazotumia umeme watembelee ofisi zetu mahali kokote nchini ili kupata huduma zetu kwani sisi tumejipanga kutoa huduma bora zaidi ya sasa"amesema dakta Kihamba
Meneja wa mradi huo Muhandisi James Masawe amesema kuwa mradi huo umeanza utekelezaji wake januari 10 ,2019 na unatarajiwa kukamilika septemba 14,2020 ambapo gharama za mradi huo ni shilingi billion 48.8 ambapo umefikia asimilia 95 katika utekelezaji wake.
"Kwa sasa kazi zinazoendelea ni kufanya majaribio ya mwisho ya mitamo ambayo imefungwa na tunarajia tahehe 14 kuwasha rasmi mitambo hii na kuwapeleka umeme wateja wetu wote katika mkoa wa Geita na wilaya za Mkoa jirani wa kagera ambapo jumla ya vijiji 10 vinapitiwa na Mradi huu ambao utekelezaji wake umefikia asilimia 100 "
Massawe amesema kuwa wakati wa utekelezaji wa mradi huo wamekumbana na mvua nyingi na kupelekea kupunguza muda wa utendaji pamoja na baadhi ya watalaamu wa ufungaji wa mashine kushindwa kufika kwa wakati kutokana na zuio la ndege lililosababishwa na uwepo wa ugonjwa wa Covid-19 ambapo kwa sasa wamewasili ili kukamilisha zoezi hilo.
Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme nchini Dk. Alexender Kiyaruzi akipokea maelezo ya mradi huo toka kwa mmoja wa watalaam toka Tanesco wakati wa ziara yao ya kukagua ujenzi wa kituo kidogo kilichopo Bulyanhulu Kahama
Ukaguzi wa kituo cha Umeme (Substation)Bulyanhulu ukiendelea
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Tanesco pamoja na wajumbe wa kamatui hiyo wakiendelea kuangalia namna ambavyo ujenzi huo unavyoendelea katika eneo la Bulyanhulu Kakora Kahama
Juu ni Mojawapo ya nguzo za umeme ambazo zimesimikwa katika kituo hicho.
eneo ambalo lilikuwa likitumika awali na kupokea umeme mdogo ambao ulikuwa haukidhi hitaji la mkoa wa Geita na wateja
Mitambo Mipya na ya Kisasa ya shirika la umeme iliyopo kwenye kituo hicho cha Bulyanhulu wilayani Kahama ambapo wajumbe wa bodi na mwenyekti wa bodi wametembelea kuona namna kinavyoendelea na kuridhishwa na ujenzi huo ambao umefikia asilimia 98
Mfumo wa ndani amabao ni mitambo ya kupokea na kusambaza umeme ikiwa ndani eneo maaalum kwa ajili ya kazi ya kupeleka umeme