Kulia ni Kaimu Kamishina wa Wanyamapori nchini Mabula Nyanda akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka nchini Biswalo Mganga hati ya makabidhiano ya jengo lililokuwa likitumika na Mamlaka ya wanyamapori kanda ya Kigosi na kupewa kwa muda litumike kama ofisi ya DPP wilaya ya Kahama.
Mamlaka ya Wanyamapori
Tanzania (TAWA) imeikabidhi ofisi ya taifa ya Mashitaka chini ya
DPP jengo lililokuwa likitumiwa na
mamlaka hiyo kanda ya Kigosi lililopo wilayani kahama mkoani Shinyanga, baada ya mapori waliyokuwa
wakiyasimamia kupandishwa hadhi na kuwa hifadhi za taifa ambapo jengo hilo litatumika
kuendesha kesi za jinai ikiwa ni mkakati wa serikali wa kupunguza Msongamano
wa maabusu na waafungwa katika Magereza nchini.
Akizugumza Jana baada ya Makabidhiano ya jengo hilo Kaimu Kamishina
wa uhifadhi nchini Mabula Nyanda amesema
kuwa kutokana na uhusiano uliopo kati
ya ofisi yake na ofisi ya DPP wamekuwa wakishirikiana katika masuala ya
uendeshaji wa kesi za makosa yaliyokuwa
yakihusika na rasimali za wanyama pori ambapo wameamua kuwapatia jengo
hilo kwa muda ili waweze kusaidia jamii katika kesi mbalimbali
“Kama mnavyojua moja ya kazi muhimu sana katika taasisi hizi
ni ulinzi wa rasimali za wanyamapori ambazo ni kazi za hima sheria ziko nne kwanza kuna operation, ukusanyaji wa taarifa, uendeshaji wa
mashitaka na upelelezi hizi zote zinahusika na mashitaka,”amesema Kaimu Kamishina Nyanda
Amesema kuwa wamekuwa wakishirikiana sana na ofisi ya taifa
ya mashitaka katika kesi zote ikiwemo zinazohusu usimamizi wa rasilimali za
wanyamapori ambapo DPP amekuwa msaada mkubwa wa kupambana na uharifu
kwenye ujangili,mifugo na uvamizi wa
mapori ya akiba hivyo tumeona umuhimu wa kuwapa jengo hili.
“Sisi tulikuwa tunatumia ofisi hii ya Kanda ya kigosi toka
hapa Kahama baadae serikali ikapandisha hadhi mapori hayo toka pori la akiba
hadi kuwa hifadhi, hivyo tukaaamua
kupisha na tulikuwa na mpango wa kuwekeza
mradi, ndipo tukapokea maombi toka kwa mdau wetu muhimu ofisi ya DPP
wakitaka tuwapatie kwa ajili ya kufungua ofisi ya taifa ya mashitaka ya wilaya ya kahama nasi hatukuwa na shida tukaamua kumpa kwa muda
kwa ajili ya utekeleza wa kazi zake za kuhudumia wananchi”
Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka nchini Biswalo Mganga amesema
kuwa kutokana na idadi kubwa ya watu walikuwa wakisafiri kwenda kupata huduma
mkoani Shinyanga hali ambayo ilikuwa
inachangia kuchelewa kutolewa kwa maamuzi hivyo kusogezwa kwa huduma hiyo
wilayani kahama itasaidia kupunguza adha ya kusafiri umbali mrefu.
“Tumeamua kufungua ofisi hapa kwa sababu gereza la kahama
linapokea watu wengi linapokea kutoka wilaya jirani za Mbogwe na
Bukombe zilizoko Mkoani Geita hivyo kuna kesi ambazo hazina ulazima sana
wakili wa serikali atazichuja na kuzitoleea maamuzi na yale yanayoshindikana
yanakuja kwetu”
Biswalo amesema kuwa uwepo wa ofisi hiyo wilayani kahama utasaidia
kupunguza Msongamano ulioko kwenye gereza hilo pamoja na
kuhakikisha kwamba kesi zinaendeshwa mapema na kwa mujibu wa sheria huku ofisi
yake ikiendelea na mkakati wa kuwa na majengo yake.
Naibu Katibu Mkuu wizara ya katiba na sheria Amon Mpanju
amesema kuwa nchi haiwezi kuwa na amani pasipo uwepo wa ofisi ya Taifa ya
mashitaka hivyo uwepo wake ni muhimu sana katika kuhakikisha
amani inadumu huku akibainisha kuwa mara
baada ya kutembelea gereza la kahama ni
jambo jema lililofanywa na DPP la kuomba kupewa jingo kwa ajili ya kuanzisha
ofisi hiyo.
“Ni vema ushirikiano huu ukaendelezwa kati ya TAWA na ofisi ya Mashitaka nchini kuhakikisha Ulinzi wa Rasilimali za nchi zinaendelea
kulindwa na kutunzwa kwa mujibu wa sheria za nchi nimefurahi sana kwa hili
lililofanyika leo kuamua kuwapa jengo hili ofisi ya Mashitaka nanyi hakikisheni
mnalitunza ili hata mkiondoka libaki katika ubora wake”
Naye katibu tawala wa wilaya ya Kahama, Timothy Ndanya amesema kuwa kwa sasa wilaya hiyo ina idadi kubwa ya wakazi takribani milioni moja hali
inayochangia kuongeza vitendo vya uharifu na ongezeko la makosa ya jinai hivyo
uwepo wa Ofisi hiyo utasiadia kuondoa
kero kwa wananchi ikiwemo ucheleweshwaji
wa kesi.
Mkuu wa Magereza Mkoani Shinyanga, Kamishina Msaidizi
Elizabeth Mbezi amesema iwapo itaanza kufanya kazi ofisi ya mshitaka ya taifa wilayani Kahama itasiadia kupunguza kesi za watuhumiwa ambao hawana ulazima sana wa kukaa
gerezani pamoja kupunguza Msongamano wa Mahabusu ndani ya gereza
“Kwa sababu Gereza
letu la Kahama linapokea watuhumiwa toka halmashauri tatu wa wilaya hii pamoja
na wilaya jirani za Mbogwe na Bukombe ambao hutumia gereza hilo kwa hiyo ifsis
hii itasiadia kurahisisha mahabusu ambao si lazima kwenda gerezani kesi zao
zikaishia nje”amesema Mbezi.
habari picha
Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka nchini(DPP) Biswalo Mganga akizungumza na viongozi na watendaji wa Tawa hawapo pichani.
baadhi ya watendaji wa ofisi ya Mashitaka na ofisi ya mamlaka ya wanyamapori wasikiliza maelezo ya namna kukabidhiana jengo hilo
Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka nchini(DPP) Biswalo Mganga akisaini hati ya makabidhiano ya jengo pamoja na Kaimu Kamishina wa Wanyamapori nchini(TAWA) Mabula Nyanda mbele ya Naibu katibu Mkuu wizara ya katiba na Sheria Amon Mpanju
Naibu katibu Mkuu wizara ya katiba na Sheria Amon Mpanju akizungumza na viongozi na watendaji wa ofisi za DPP,Tawa na Ofisi ya upelelezi Mkoa wa Shinyanga na Wilaya ya Kahama
kamishina Msaidizi Mwandamizi mamlaka ya Wanyamapori nchini (TAWA) akieleza mambo mbalimbali juu ya ushirikiano wao na Ofisi ya (DPP) katika kuendesha Kesi
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Mashitaka Nchini (DPP) Edson Makallo akizungumza namna ambavyo ofisi yake itaklitunza vizuri jengo hilo ili liweze kutoa hduma zilizokusudiwa na wananchi kupata haki mapema
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Amon Mpanju walio kaa kwenye wa tatu kutoka Kushoto akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya makabidhiano ya jengo litakalotumiwa na ofisi ya DPP wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga
jengo la mamlaka ya wanyama pori lililokuwa likitumiwa kama ofisi ya kanda ya kigosi baada ya baadhi ya mapori yaliyokuwa yakisimamiwa kupandishwa hadhi na kuwa hifadhi za taifa sasa limekabidhiwa kwa mwendesha mashitaka mkuu wa serikali DPP ili liweze kutumika kutoa huduma kwa wakazi wa Kahama,Mbogwe na Bukombe ili kupunguza msongamano kwa maabusu katika Gereza la Wilaya ya Kahama.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464