UMMY MWALIMU AAHIDI NEEMA KWA WAVUVI TANGA

 
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kushoto akimnadi mgombea Udiwani wa Kata ya Tangasisi Jijini Tanga wakati wa mkutano wake wa kampeni 

WAVUVI Jijini Tanga wamehaidiwa kupatiwa neema ya kusaidiwa kupata dhana za kisasa ikiwemo kuimarisha umoja wao ili waweze kupata mafanikio makubwa kupitia sekta hiyo.


Hayo yalibainishwa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wake wa kampeni Kata ya Tangasisi Jijini Tanga.


Alisema kwamba ataimarisha umoja huo ili wavuvi waweze kuvua kisasa hatua ambayo itawasaidia kuweza kupata samaki na kuweza kujikwamua kiuchumi wao na jamii zao na hatimaye kukuza kipato chao


“Ndugu zangu wavuvi nitahakikisha mnapata dhana za kisasa lakini pia kuimarisha umoja wenu katika kata ya Tanga sisi na Jiji lote la Tanga muweze kupata mikopo isiyo na riba na kununua vifaa vya uvuvi vya kisasa”Alisema


Akizungumzia suala la fidia ya barabara Kata ya Tangasisi hadi Mwahako alisema tayari alikwisha kuongea na Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Tanga (Tanroad) na tathimini inaendelea ikikamilika watu wote ambao wapo barabarani watapata malipo.


“Ndugu zangu ninatambua hapa Tanga sisi hadi Mwahako kuna suala la fidia ya Barabara suala hili tayari nimekwisha kuzungumza na Meneja wa Tanroad Mkoa wa Tanga tayati tathimini inaendelea ikikamilika watu wote mliopo barabarani mtapata malipo yenu”Alisema 


Hivyo aliwaomba wamchague kwa sababu ya uchungu alionao wa kuionga Tanga iweze kusonga mbele huku akiwataka wampe kuwa nyingi za ndio kwa sababu amedhamiria kuibadilisha Tanga.


Awali akizungumza katika mkutano hyo Katibu wa UWT Mkoa wa Tanga Sophia Nkupe aliwaomba wapiga kura kumchagua mgombea ubunge wa Jimbo  la Tanga Ummy Mwalimu kwa sababu amelelewa na jumuiya hiyo.


“Lakini pia Ummy Mwalimu ni tunu kubwa tulioipata na kiongozi jasiri mwenye mafanikio hivyo wananchi hatupaswi kufanya makosa kwa kuipoteza”Alisema


“Ndugu zangu Ummy Mwalimu ni tunu kubwa tuliopata hivyo wananchi na wana Tanga hatupaswi kufanya makosa wakati wa uchaguzi mkuu tumpeni kura nyingi za ndio aweze kuilipatisha Jiji letu kutokana na mipango mizuri aliyonayo “Alisema


Katibu huyo aliwaomba wananchi hao kuhakikisha wana mpa kura za kishindo Rais Dkt John Magufuli ,Ummy Mwalimu na Diwani ili waweze kuchochea kasi ya ukuaji wa maendeleo kwao
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto akiwatubia wananchi wa Kata ya Tangasisi wakati wa mkutano wake wa kampeni

KATIBU wa UWT mkoa wa Tanga Sophia Nkupe akimuombea kura Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu wakati wa mkutano huo
KATIBU Mwenezi wa CCM wilaya ya Tanga Lupakisyo Kapange akmuombea kura Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu 
Msanii Mchina Mweusi akitumbuiza wakati wa kampeni hizo


MWENYEKITI wea Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Tanga Nassoro Makau akiwa na Mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa Mbaruku Asilia wakifuatilia mkutano wa mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu
Muwania  Udiwani viti malumu Tarafa ya Pongwe Mecha Goodluck akionyesha dole wakati akiwa kwenye mkutano wa mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu
MUWANIA Udiwani wa Viti Maalumu Tarafa ya Pongwe Mecha Goodluck Matile akimuombea kura mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia wakati wa mkutano huo
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akiwa ameshika mtoto mara baada ya kumaliza mkutano wake wa kampeni Kata ya Tangasisi 
Umati mkubwa wa wananchi waliofurika kumsikiliza mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kata ya Tangasisi Tanga
Umati mkubwa wa wananchi waliofurika kumsikiliza mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kata ya Tangasisi Tanga
Umati mkubwa wa wananchi waliofurika kumsikiliza mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kata ya Tangasisi Tanga
Team Ummy Mwalimu wakiwa kwenye mkutano wa hadhara Kata ya Tangasisi 
Msanii wa mziki wa Bongofleva Mwandeya akitumbuiza wakati wa kampeni hizo

Msanii Kasimu Mganga akitumbuiza wakati wa mkutano huo 


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464