VIONGOZI na Wajumbe wa bodi ya chama cha msingi (AMCOS) cha Mwananchi wilayani Kaliua mkoa wa Tabora wamekubali kurejesha kiasi cha Sh Milioni 23,124,613.05 ambazo ni za chama hicho zilizolipwa na viongozi hao kinyume na utaratibu na kuamua kuzigawa kwa maslahi yao binafsi.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Septemba 18, 2020 na Mkuu wa Takukuru mkoa wa Tabora, Mussa Chaulo imesema kwamba watuhumiwa hao mpaka sasa wamerejesha Sh Milioni 15,502,050 baada ya Takukuru kufuatilia tuhuma za malipo hayo hewa.